Bashe: Mpina huyu aliua Kitalu cha Mbegu kwa Siasa za Uongo, alimpotosha Rais Magufuli

Bashe: Mpina huyu aliua Kitalu cha Mbegu kwa Siasa za Uongo, alimpotosha Rais Magufuli

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, akihutubia Mkutano wa Hadhara Wilaya ya Meatu Mkoa wa Simiyu, leo tarehe 17 Juni, 2025 kwenye ziara ya Rais samia amesema kuwa;

''Jambo jingine ambalo Mhe. Rais nataka nilitolee maelezo na nataka hili niliongee polepole Wakulima wote wa Pamba na Wanasiasa wenzangu wanielewe katika hili. Mhe. Rais toka historia ya nchi hii Mkulima wa Simiyu alikuwa anapata Kilo 200 na 300, Wanasiasa wa Mkoa wa simiyu wameitumia Pamba kama Siasa na sio zao la Kiuchumi la kuwatoa watu katika Umasikini"

"Hakuna mtu yeyote anayeweza kutathimini bei ya Pamba isipokuwa Serikali hata wakiwa wanunuzi 500 kwenye Kijiji bei ya Pamba inaamuliwa na Serikali"

"Nataka nimuombea ndugu yangu Mpina hapa, mbele ya Wanazengo, mimi na yeye tulishakubaliana Mhe. Rais, atasema Hoja zake nitazijibu hadharani kwasababu hakuna Serikali ambalo inaficha"

"Mpina huyu aliua Kitalu cha Mbegu katika Kijiji cha Mobusalu kwa Siasa hizi hizi za kuwadanganya wananchi"
 
Back
Top Bottom