Suzy Elias
JF-Expert Member
- Nov 9, 2021
- 1,067
- 6,200
Bwana mdogo Bashe kwa siku za hivi karibuni umeonyesha hali ya kujiamini iliyopitiliza huku ukisahau kwamba wewe ni mteule na mda wowote uteule wako unaweza kutenguliwa.
Tatizo la vijana wengi huwa mnavimba vichwa mnapopata kuaminiwa na kusifiwa na mteule japo kwa mambo kadha wa kadha mnapotimiza wajibu wenu mfano ni wewe Bashe na wenzako kama kina January.
Wadogo zetu timizeni wajibu wenu pasi na kuvimba kichwa huku mkijibu kwa mbwembwe na nyodo wenzenu wasiyo na madaraka kama yenu.
Yupo wapi leo mjivuni Kigwangala na mbwembwe zake?!
Yupo wapi leo Mpina na ulijali wake?!
Funzo hapa ni muhimu na lazima muwe welevu na muwiwe na kiasi. Madaraka ni dhamana tu na aliyekupa anaweza kukunyang'anya pia.