Bashe umefeli juu ya suala la chakula

Bashe umefeli juu ya suala la chakula

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Acha porojo mbovu. Kama mnakusanya tani laki tano ya vyakula mbona mfumuko wa bei za vyakula upo juu?

====
Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe amesema uwezo wa kuhifadhi chakula umeongezeka kutoka tani laki 200,000 mpaka laki 500,000 hivyo wakati wa msimu wa kuvuna watanunua mahindi na mpunga kiasi cha kutosha ili kujiweka sawa kama kutatokea mazingira ya uhaba wa chakula.

"Mazao ya wakulima ni mali yao wanahaki ya kuyauza popote na sisi serikali hatutazuia mkulima kuuza mazao yake popote kwani kwa muda mrefu wamekuwa maskini kwa manufaa ya watu wengine"_ Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe

Serikali imesema haitaondoa mfumuko wa bei za mazao kwa kumtia umaskini mkulima bali itachukua hatua kuhakikisha kuwa mlaji naye analindwa.Pia imesema itahakikisha inaweka uwiano wa mazao ya chakula kwa kuingiza chakula sokoni kwani kama serikali huo ndio muelekeo watakaouchukua.

Image
 
Vyakula kupanda ni sababu ya ukame, sio Bashe

Mwaka 2017 kilo ya unga ilifika 2200, unga ukawa ghali kuliko mchele

Mwaka huu kuanzia mwezi March/April mahindi na mchele mpya vinaingia sokoni na bei zitashuka

Hili halihitaji hata akili nyingi kujua, sema watu mnapenda siasa za hovyo tu
 
Vyakula kupanda ni sababu ya ukame, sio Bashe

Mwaka 2017 kilo ya unga ilifika 2200, unga ukawa ghali kuliko mahindi

Mwaka huu kuanzia mwezi March mahindi na mchele mpya vinaingia sokoni na bei zitashuka

Hujui lolote.
 
Ukame wakati hayo mahindi bei inapanda yakiwa yapo katika maghala ya serikali

Kama nchi ingekuwa imekumbwa na ukame basi katika maghala yetu kusingekuwa na nafaka na serikali ingetoa vibali Kwa wafanya biashara kuagiza nafaka kutoka nje kama inavyofanya Kenya

Nafaka zipo za kutosha zimejaa katika maghala yote ya serikali lakini Kila siku bei inapanda huo ni uzembe wa waziri mwenye dhamana na anawanufaisha mafisadi na kuwaumiza wananchi
 
Acha porojo mbovu. Kama mnakusanya tani laki tano ya vyakula mbona mfumuko wa bei za vyakula upo juu?View attachment 2500551
T
Ni uamuzi mzuri sana ambao umechelewa ila utaleta matunda miaka ijayo. Ni <15% ya ardhi yenye rutuba ndiyo inalimwa Tanzania. Watu wengi wamejikita kwenye uchuuzi na umachinga mitaani.

Maamuzi ya Bashe ni FURSA ambayo wenye AKILI tayari wanakimbilia vijijini kwenda kulima. Ila WAPUMBAVU watabakia JF kuandika threads za kutaka mipaka ifungwe ili wavivu waendelee kununua unga kwa Tsh 1,000.

Shikilia hapo hapo Bashe, wakulima waamue wenyewe wauze wapi na siyo kupangiwa na wavivu
 
Ndio na ndio sababu kilidumaa na hakuna serikali ilikipa kipaombele isipokuwa awamu ya 6..

Hayo mengine ni porojo zenu zisizo na maana ,Jiwe ndio aliua Kila kitu..
Acha uzushi, scheme nyingi za Umwagiliaji zilijengwa wakati wa Mwalimu na Watanzania wengi walisomeshwa kwa pesa ya Kilimo na Wakulima waliuza mazao yao kupitia vyama vya ushirika.
Kilimo kilianza kufa wakati wa Mwinyi,Mkapa na Kikwete walifanya maziko.Magufuli aliondoa matokeo kibao ya mazao ya Wakulima.Sasa Samia yeye kafanya kipi kwenye Kilimo cha kumsifia!!!
 
T
Ni uamuzi mzuri sana ambao umechelewa ila utaleta matunda miaka ijayo. Ni <15% ya ardhi yenye rutuba ndiyo inalimwa Tanzania. Watu wengi wamejikita kwenye uchuuzi na umachinga mitaani.

Maamuzi ya Bashe ni FURSA ambayo wenye AKILI tayari wanakimbilia vijijini kwenda kulima. Ila WAPUMBAVU watabakia JF kuandika threads za kutaka mipaka ifungwe ili wavivu waendelee kununua unga kwa Tsh 1,000.

Shikilia hapo hapo Bashe, wakulima waamue wenyewe wauze wapi na siyo kupangiwa na wavivu
Sasa kama sasa hivi mnakusanya tani laki tano bei ingeshuka. Mngeuza nje na ndani chakula kikawa kingi
 
Acha porojo mbovu. Kama mnakusanya tani laki tano ya vyakula mbona mfumuko wa bei za vyakula upo juu?

====
Waziri wa kilimo Mhe.Hussein Bashe amesema uwezo wa kuhifadhi chakula umeongezeka kutoka tani laki 200,000 mpaka laki 500,000 hivyo wakati wa msimu wa kuvuna watanunua mahindi na mpunga kiasi cha kutosha ili kujiweka sawa kama kutatokea mazingira ya uhaba wa chakula.

"Mazao ya wakulima ni mali yao wanahaki ya kuyauza popote na sisi serikali hatutazuia mkulima kuuza mazao yake popote kwani kwa muda mrefu wamekuwa maskini kwa manufaa ya watu wengine"_ Waziri wa Kilimo Mhe Hussein Bashe

Serikali imesema haitaondoa mfumuko wa bei za mazao kwa kumtia umaskini mkulima bali itachukua hatua kuhakikisha kuwa mlaji naye analindwa.Pia imesema itahakikisha inaweka uwiano wa mazao ya chakula kwa kuingiza chakula sokoni kwani kama serikali huo ndio muelekeo watakaouchukua.
Image
Sijui una elimu au experience gani ya uchumi
 
Vyakula kupanda ni sababu ya ukame, sio Bashe

Mwaka 2017 kilo ya unga ilifika 2200, unga ukawa ghali kuliko mahindi

Mwaka huu kuanzia mwezi March mahindi na mchele mpya vinaingia sokoni na bei zitashuka

Hili halihitaji hata akili nyingi kujua, sema watu mnapenda siasa za hovyo tu
Unga ghali kuliko mahibdi ??!!!!
 
Huyu ni mmoja kati ya vijana wenye akili sana hapa Tanzania.

Mkulima aheshimiwe, kama hauridhiki shika jembe ukalime

Wakulima ndiyo kundi kubwa la wawekezaji wazawa na ni sehemu kubwa ya population yetu, kama mapato yao yakiongezeka maana yake tumenyanyua GDP yetu na pato la wastani la kila mtanzania.

Hii, ina translate ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa purchasing power.

Ni wewe na kundi la wapumbavu wenzako mnaowaza kwa kutumia makalio na msiotakia taifa hili mema, mnadhani huyo dogo amefeli, yuko timamu.
 
Free trade rules unazijua?

Au ndio keyboarding and betting tu
We fala unadhani kila mtu ni makalio kama wewe? Kama una ziada ya tani laki tatu sasa huu mfumuko utokee wapi?
 
Back
Top Bottom