Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Wakuu,
Aprili 7, 2017 Bashe aliandika haya kupitia ukurasa wake wa Twitter (X), "Sote tusimame tuseme hapana kwa mfumo huu unaoanza kuota mizizi. Kama mtu ana makosa ufatwe utaratibu wa kisheria kumkamata sio utekaji."
April 10 akiwa bungeni aliweka hoja mezani akiomba bunge liahirishe shughuli zake ili kujadili suala la utekaji ambalo lilikuwa linazidi kushamili akitolea mfano ambao wamewahi kupitia kashkash za kutekwa ikiwemo yeye mwenyewe Bashe, Sugu, Malima, Musukuma, Roma, huku wengine kama Ben Saanane wakiwa hawajulikani wapo.
Akisema kuna kikundi ndani ya usalama wa taifa ambao ndio wanateka watu na kutia doa serikali, nchi na chama, na serikali imekaa kimya!
Aprili 7, 2017 Bashe aliandika haya kupitia ukurasa wake wa Twitter (X), "Sote tusimame tuseme hapana kwa mfumo huu unaoanza kuota mizizi. Kama mtu ana makosa ufatwe utaratibu wa kisheria kumkamata sio utekaji."
Akisema kuna kikundi ndani ya usalama wa taifa ambao ndio wanateka watu na kutia doa serikali, nchi na chama, na serikali imekaa kimya!
Leo hii Bashe anaweza kunyanyua kinywa chake na kuongea haya? Anaweza kutetea Watanzania wanaotekwa ovyo sababu ya kukosoa serikali, chama chake pamoja na/au Rais? Bashe huyu kapotelea wapi? Hayaoni haya yanayotekea sasa? Haoni huu uonevu unaoendelea?