Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

Facts.. Ila shida itakua ni kwenye utekelezaji na hasa ukizingatia kwamba hata kwenye kampuni ya serikali (TTCL) hilo tatzo lipo.. Ila nakuombea ushindi mdau ili iwe faida kwako na Taifa kwa ujumla
 
Dah! Elfu sitini kwa wiki moja nailikuwa iwe kifurushi cha mwezi! Sitasahau!
 
Suala hili lilianzia KENYA kwa baadhi ya wadau kuishitaki safaricom, na wako katika mchakato mzuri wa kuifanikiwa. Ni vizuri kuAdapt walichokifanya wakenya but ushauri wangu kwako inabidi ufuatilie kwa undani kuhusu business law ya telecommunications company kwasababu na wao wenyewe wana-operate kwa sheria zao compared to their business strategies.

Ni wazo zuri but you need to do follow up,otherwise utafeli mahakamani, kingine jaribu kucheki na wakenya strategy yao against safaricom
 
Nilijiuliza sana inakuwaje unanua bundle hata ujalitumia kutokana na ubisy unambiwa limexpire kwangu mimi nachukulia kama ujanjajanja.Bando nikishanunua sipaswi kufungwa na mda wa kulitumia mimi napaswa nitumie mpaka liishe.Wakili tuwakilishe vema.
 
Unajua iko hivi wanapokupa dakika 20 kwa shilingi 1000 maana yake wamekupa chini ya bei halisi Yaani wamekupa dakika moja kwa shilingi 50 sawa Na sekunde moja kwa shilingi 0.833
wakati uhalisia ni shilingi 400 kwa dakika moja Yaani Shilingi 6.66 kwa sekunde sasa kwa vile ni offer ndio maana wanapanga muda ili kujinufaisha Na wao
Yaani iwapo wateja kumi wakijiunga Na wote wakatumia muda wao kamili basi imekula kwao Lakini wakatumia nusu tu basi na wao wanafaidika pia ni Kama bahati nasibu vile
Haya ni maoni yangu tu Nadhani tujiandae Na majibu kama Hayo kutoka kwao
 
Nonesense
 
Kuna kitu watu wengi hawakijui mitandao ya simu haipati hasara kwenye vifurushi kuanzia sms, dakika na Mbs hii ni mtego wa kurudisha gharama za equipment installation, kiuendeshaji (maintanance na operation costs) zirudi na cha juu ambayo ndiyo faida yao so huu mchezo wameuzoea hapa Tanzania ndiyo maana 3G tunadanganywa ni 4G waliowahi kutumia data abroad wanaelewa
 
watu wanapenda bure Sana Lakini ukweli ni kwamba gharama za simu hapa ukilinganisha Na nchi nyingine sie tuna nafuu mara mia kuliko Wengi ne
basi sijui Tunakwama wapi
 
Bashir Yakub,
Well done msomi wetu. Mimi binafsi niko tayari kuunganishwa/kujiunganisha kwenye hii kesi ya kudai hizo haki zinazokiukwa na haya makampuni ya huduma au hujuma za mawasiliano. Halafu, kuna wakati huwa nashanga na kujiuliza, kwani mambo kama hayo uliyoanisha hapo juu, kweli hawa ndugu zetu wa TCRA NA TUME YA HAKI ZA WATEJA WA MAWASILIANO, hawayaoni au hawayajui au wanayafumbia macho kwa maslahi yao wenyewe? Tafadhari zidi kutupa feedback on the development of this important issue. Asante sana msomi.
 
Tanzania inaongoza kwa kutoza viwango vikubwa vya intaneti katika nchi za Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa cable.co.uk,Zimbabwe inangoza duniani kwa na gharama za intaneti ambapo gigabaiti 1(1GB) inagharimu dola za kimarekani 75.2 (TZS.172,847),ikifuatiwa na Equatorial Guinea dola za kimarekani 65.83.
India inaongoza kwa kuwa na kiwango kidogo ambapo1GB ni dola za kimarekani 0.26 (TZS.598).
Huku Tanzania ikiongoza kwa gharama kubwa Afrika Mashariki na Kati.
 
Ndugu Bashir Yakub nafurahi kugundua kuwa Lengo lako ni kuwa mmoja wa wapigania haki za wanyonge. Iko gudi.

Nina mashaka na hoja zako (numbered) Kwa nini?.... Ni kwamba umefaninisha kifurushi tunachokupatia (mf. Wajanja night) na vifurushi vya luku, maji nk of which is quite wrong. Kivipi.... Naomba ukumbuke kifurushi tunachokupatia kama voda/tigo/airtel ni OFFER ambapo usipotaka kutumia offer ninayokupa utalazimika kutumia muda wako wa hewani wa kawaida (prepaid or postpaid ). So it's just an offer ambayo ni tofauti na luku au dawasa
Sasa mpaka ukae mkao wa biashara ndo utaelewa ila uking'ang'ania uwakili wako tu kwa hoja hizo ulizoainisha utakusumbua.
Sasa basi kama offer tuna uhuru wa kucustomize offer zetu, kivipi? Ni kwa kukuwekea pia span ya kifurushi. So ni kitu unayoeza kuona from business point of view.

-Swala jingine umezungumzia haki kutochanganya kifurushi na muda wa kawaida wa hewani. Sasa anayechanganya hayo ni mimi (voda/tigo ) au wewe?
Wewe ndo unayeruhusu kwenye simu yako au device yoyote similar to that maana kwenye simu ndo unaeza turn ON or OFF data. Ukiacha ON mimi kama service provider nitatambua kuwa bado unahitaji kuwa mtandaoni ninachokifanya naangalia kama unavigezo kwa aidha kifurushi au salio lako kawaida kama vipo utaendelea kusurf tu bablai. Sasa unataka nikuamulie tena eti sasa ivi Zima data kifurushi kimeisha haah! !!

Sasa wengi jukwaani humu watakusupot kwa sababu (kwa kutotambua wajibu wao) walipigwa na mitandao hiyo.
Hizo sheria unazozijua ukitumia vibaya tunakufunga wewe mwenyewe. So try to have wide overview/perception of your topic.

Kuna eneo uko sahihi nimeona nisilizungumzie.

Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…