Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

Naomba nikupe ushahidi mkuu
 
Watakutafuta watakupenyezea bahasha nia ya kuendelea na kesi itaishia hapo mlevi mmoja alijisemea.

Turudi kwenye mada... Mimi nakutakia kila la kheri ushinde kesi ktk vipengele vyote na vingine ambavyo mahakama itaona vinafaa kubadilishwa
 
kigogo kalenga mule mule hata Mkuu Baba Jiwe kwa hili atalibariki

sema tu hatoagi mailege so atayaamuru kimya kimya
 
Wazo zuri, na umedadavua haswa japo watakwambia wameweka kifurushi cha bila ukomo. Kwa jicho la kiuchumi kwao watashuka kimapato, kinyume chake itakuwa nafuu kwa mteja.

Mkuu sisi wote ni walaji lakini bwana afya wetu na mlinzi wa afya zetu (TCRA) ndio huyooo anagonga glass na muuzaji je unategemea nini hapo?
 
Huku nchi jirani niliko kwa huu mtandao ninaotumia uko na hizo huduma zote.

Ikiwa umejiunga na kifurushi chako chá mb na umeacha hela basi hela yako haiendi na na utapewa tarifa kabla ya muda wko kuisha kabisa.

Unapokuwa na SMS za ziada unaweza kuzibadilisha Muda WA maongezi au MB.

Unaweza pia kumtumia mtu mg kiwango unachotaka.
 
Juzi nimeweka vocha ya 1000 ya Halotel. Wakakata 381 wakanibakizia 619. Nikapata hasira sana hapo ni saa 5 usiku. Nikabidi nijiunge na kifurushi cha 500. Asubuhi nikawapigia simu. Nilichoka kwa majibu yao. Wanadai nilijiunga na kifurushi cha 500 na tena nikajiunga na kifurushi cha 400. Siwezi tena kununua vocha ya Halotel, nitaweka kupitia Halopesa.
Mto uzi upo sahihi. Naunga na wewe maana wanafanya wizi. Unanunua kifurushi halafu wanakupangia muda wa kutumia. Pesa yangu halafu unipe na muda wa kutumia.
 
Daa hii kweli si haki kabisa yaani mkuu endekea na hizo halakati tuko pamoja nawe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…