Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

Bashir Yakub: Nitayashitaki makampuni manne ya simu

TheChoji,
Jiwe aliwapandishia kodi, nao wamegundua namna ya kutuibia, awamu hii ina wizi sana kuliko ya KIKWETE NA MKAPA, JAPO KWA MKAPA WIZI WA KUUZIANA NYUMBA ZA SERIKALI HAUTA KAA KUSAHAULIKA VIZAZI NA VIZAZI
 
Ambao tumewahi kununua kifurushi cha buku mbili voda kwa njia ya m-pesa alafu m-pesa yako inakatwa na kifurushi hupati na customer care huwapati...tunacomment uzi huu huu?
KAWAIDA sana hiyo, unanunua bando la 2000 ukiweka data on hata sms za watsup haziingii
 
Halotel kwenye vifurush vya mb ni wezi wakubwa, labda utumie kwenye simu ila ukitumia computer, Gb 1 haikai hata lisaa tofauti na mitandao mingine, na hapo sijasema kama mitandao mingine hawaibi ila si kama halotel asee
Halotel ni ashushushu toka vietnam, wanajua kuiba na mitambo ya TCRA wameshindwa kunasa, hii nchi ni shamba la bibi
 
jaji mfawidhi,
Kwasie tulioanza kutumia simu zamani,enzi hizo unanua dollar na nikilinganisha kwa sasa aisee gharama za sasa ni nafuu sana baada ya kuja kwa vifurushi....Ndio maana makampuni yamekuja na kifurushi unachotaka Jipimie aka size yako.

Kabla haujajiunga angalia kwanza matumizi yako kwa wiki/mwezi ni kihasi gani,jaribu kufanya utafiti kwa miezi ateast mitatu kuweza kujua matumizi sahihi...Ukishajua matumizi yako ni GB au Dakika ngapi kwa mwezi/wiki basi jiunge kifurushi kulingana na size yako,haiwezekani wewe matumizi yako kwa wiki ni GB 2 ukajiunga kifurushi cha GB 5 huku ukitegemea ikifika wiki kampuni ikurefund GB zako 3 wakati kulikuwa na bundle ya GB 2 kwa bei ya chini.

Kuna Halichachi na offer maalumu kwa kila mitandao,kwa kifupi fanya utafiti wa kujua mtandao gani unameet your requirements,kwasasa ukisajili line tu halotel wanakupa free dakika 30 utumia kwa wiki nzima x all networks.

Ukifungua hiyo kesi yako unadondokea pua kabla hata haijafika kwa hakimu,yaani unadondoshwa kwenye level ya ushauri wa mwanasheria tu au unadondokea pua kwenye korido za TCRA.
 
Makampuni ya Tigo, Airtel, Vodacom,Zantel na Halotel kushitakiwa. Wanasheria naombeni ujuzi wa hili suala.


NAYASHITAKI MAKAMPUNI MANNE YA SIMU.

BASHIR YAKUB, Wakili.
0714047241

Naishitaki Tigo, Airtel, Vodacom, Zantel na Halotel. Kwa mujibu ya Sheria Namba 12/2003 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania mashtaka ya aina hii natakiwa kuyaandikia makampuni hayo taarifa kuyataka yarekebishe ndani ya siku 30 ninacholalamikia yakishindwa naendelea mbele,ambapo nimeshayaandikia makampuni hayo.

Kwenye mashitaka yangu ninaomba mambo matano.

JAMBO LA KWANZA. Vifurushi vyote havipaswi kuexpire. Kitu pekee ambacho kinapaswa kumaliza kifurushi inatakiwa iwe ni wewe kuongea hadi dakika zako zikaisha.

Si haki kukata kifurushi cha mtu ambaye dakika zake za kuongea,za data, au sms bado zipo kwa kigezo cha kuexpire au muda wake wa wiki,masaa12,nk kuisha. Nchi nyingi hii kitu imeondolewa imebaki kwetu na pengine pachache.

Mathalan, umejiunga kifurushi cha 1000 na umepewa dakika 10 ndani ya masaa 12. Umetumia dakika 3 tu ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 300, na masaa 12 yameisha. Maana yake kwenye 1000 yako zilibaki dakika 7 ambazo thamani yake kifedha ni shilingi 700, ambazo hizo sasa shilingi 700 kampuni ya simu inajirudishia kwa kigezo cha muda kuexpire. Nachelea kuiita huu wizi lakini initoshe kusema hii haiwezi kuwa haki.

Lakini pia ninapolipa 500 na wewe ukaniuzia kifurushi si nimekulipa hela yako yote na wewe hunidai. Sasa kwanini tena unachukua kilekile nilichonunua kwako na hela yako yote nimeshakulipa.

Ni hivi, unaponunua kifurushi ni sawa na umenunua bidhaa, na ukishanunua bidhaa hakuna mtu mwingine yeyote, akiwemo aliyekuuzia bidhaa hiyo, mwenye haki ya kuichukua tena bidhaa hiyo yote au sehemu yake isipokuwa wewe uitumie mpaka iishe.

Tizama Tanesco na LUKU. Tanesco akishakuuzia umeme/units ukamlipa basi hatma ya units zako ni utumie mpaka umalize.Hawezi kuikata na kujirudishia kwasababu anajua alikuuzia bidhaa na wewe ukamlipa na hivyo una haki ya kutumia bidhaa yako mpaka umalize. Hii ndiyo HAKI.

Kinachofanywa na makampuni ya simu ni sawa ununue mkate dukani na mwenye duka umlipe hela yake yote. Halafu mwenye duka huyohuyo akwambie kwamba usipokula mkate huo kufikia saa 12 za jioni au ndani wiki au mwezi nitakuja tena kuuchukua nyumbani kwako, na aje kweli auchukue iwe mali yake tena kwa mara ya pili.

Zaidi ya hayo,ukweli halisi ni kuwa kifurushi kwa muundo wake si bidhaa inayoexpire. Ukinunua mkate ukiexpire utauona, utaona kabisa kwa macho umeoza kadhalika bidhaa nyingine zenye sifa ya kuexpire. Lakini kifurushi kwa uhalisi wake si bidhaa inayoexpire au yenye sifa ya kuexpire.

Hili neno kuexpire limetengezwa ili kuficha neno kupora au uporaji. Ukweli ni kwamba kifurushi kinaporwa makusudi kwa kigezo hovyo kabisa na dhahania cha kuexpire, sijui masaa yako 12, sijui wiki yako, sijui mwezi wako umeisha nk. Kifurushi kinaishaje kabla dakika zangu nilizolipia kwa ukamilifu sijazitumia zikaisha ?.

Yapo haya nayo lazima yaeleweke, mtu amejiunga lakini yuko safarini hawezi kutumia mda wake , mwingine alipo hakuna network, mwingine hajatumia mda wake alikuwa bize na kazi zake, mwingine simu haikuwa na chaji siku nzima, mwingine umeme ulikatika alikosa mawasiliano nk nk, hawa wote pesa zao walizolipia na hawajazitumia au wametumia kidogo zinakatwa na makampuni ya simu yanajirudishia pesa hizo bila kujali.

Nimefungua kesi kuondoa unyonyaji huu na lazima uondoke.Hatuwezi kuendelea kuwa viwanda vya kutengeneza ukwasi wa makampuni ya simu.

JAMBO LA PILI. Haki ya kutochanganyiwa kifurushi na muda wa kawaida wa maongezi bila ridhaa.

Nitatoa mfano, unakuta mtu ameweka shilingi 1000 kwenye simu ambapo anajiunga 500 na 500 inabaki kama muda wa maongezi wa kawaida. Wakati anapokuwa akizungumza au akitumia data kupitia ule muda aliojiunga na ukaisha basi simu haikatiki bali inaunganisha moja kwa moja na ile 500 ya muda wa maongezi wa kawaida ambayo alikuwa hajajiunga.

Hii si sawa hata kidogo na ni vitu ambavyo vinatengenezwa maksudi ili kujipatia fedha bila kujali mtumiaji anaumia kiasi gani. Ni hivi, mtu anapoamua kujiunga 500 na akabakisha 500 bila kuiunga ana maana yake kubwa tu.Hakushindwa kuunganisha 1000 yote.Amechagua 500 kwa maksudi maalum. Sasa iweje unamlazimisha kutumia akiba yake ya 500 hata bila ridhaa yake.

Inatakiwa kuwe na chaguo(option) iwapo mtu anahitaji huduma ya aina hiyo au hapana. Au inatakiwa muda wa kifurushi ukiisha simu ikate halafu kama anataka kuendelea kutumia muda wa kawaida achague mwenyewe kuendelea kuutumia na sio kampuni ya simu kumchagulia.

Au kama anataka kujiunga na hiyo 500 iliyobaki basi ajiunge. Isiwe biashara ya kuviziana kama ilivyo sasa. Hili nalo lazima waliondoe.

JAMBO LA TATU, Haki ya kujua matumizi ya kifurushi. Malalamiko ya vifurushi vya watu kuliwa isivyo kawaida ni mengi mno.

Unanunua dakika 20 unaongea 10 unaambiwa kifurushi kimeisha, unabaki kushangaa. Ni lazima waweke mfumo wenye kutoa taarifa sahihi na za wazi (transparency) ili kumwezesha mtumiaji kumonita matumizi ya kifurushi chake.

Malalamiko ya watu ya kutumia vifurushi chini ya kile walichonunua yanaongezeka siku hadi siku. Kuwaachia makampuni ya simu wao wawe ndio wauzaji wa vifurushi, na wao hao hao ndio wakueleze umetumia nini,kama umemaliza au hujamaliza, huku wewe mteja ukiwa kipofu/gizani ukisubiri kupokea lolote wanalolisema wao, kupigwa hakuwezi kukwepeka.

Waweke mfumo ambao wao pamoja na mteja watamonita matumizi ili mteja aweze kuhoji. Teknolojia imekua hili ni dogo sana.

JAMBO LA NNE. Haki ya kuhamisha kifurushi.

Nimesema hapo juu kifurushi ni mali yako na ndo maana unailipia pesa na hivyo kuwa na haki ya kuitumia kwa uhuru.

Kwa msingi huu makampuni ya simu ni lazima yaweke mfumo unaomwezesha mtu kumhamishia mtu mwingine kifurushi kama ilivyo kwenye muda wa kawaida wa maongezi. Maana yake nikinunua kifurushi cha 1000 labda dakika 10 za maongezi, MB 100, na sms 50.

Niwe na uwezo wa kumgawia yeyote ninayemtaka kiasi cha muda wangu wa maongezi,sms au MB. Na hii inafanyika nchi nyingi na inawezekana zaidi kugawiana watu wa mtandao mmoja.Tunahitaji uhuru huu kwetu.

JAMBO LA TANO. Haki ya kupewa tahadhari kuhusu kifurushi au muda wa hewani unapokaribia kuisha. Kuna makampuni wana huduma hii lakini wanaitoa kwa hiari sana na wengine wameacha kabisa. Wengine wanatoa tahadhari muda unapoisha na sio unapokaribia.

Tunataka watoe unapokaribia ili mtu ajipange. Ni haki mtu kupewa tahadhari wakati akizungumza,akiwa kwenye mtandao, au sms, kuhusu dakika zake kukaribia kuisha. Sio sahihi wala ustaarabu simu kukatika ghafla bila tahadhari.

Na wanafanya hivyo maksudi wakijua unapokatakiwa na mawasiliano ghafla ni lazima tu utakuwa hujamaliza haja yako na hivyo utalazimika kuongeza vocha ili umalizie na wao wapate mauzo zaidi.

Wanajua ukipewa tahadhari unaweza tu kufupisha mazungumzo yako na wakati simu inakatika ukawa tayari umemaliza na hivyo usihitaji tena kuongeza vocha. Tabia za hovyo kabisa za kuviziana.

Unawezaje kunipa tahadhari ya muda kuisha ukashindwa kunipa ya muda kukaribia kuisha. Hili nalo tunataka lifanyiwe kazi.

SHERIA
Mambo haya kwa ujumla wake ni kinyume na Katiba ya JMT Ibara ya 18( c ) inayotaka uwepo wa mawasiliano bila kuingiliwa, lakini yanakiuka Kanuni za Kielektroniki na Mawasilano ya Posta kuhusu viwango vya Tozo GN. No 22/2018 hasa Kanuni ya 4 ( 1na 2) inayotaka viwango vyote vya tozo za simu kuwa vya haki na kadri(just and reasonable), yanakiuka Kanuni ya 4 ya Kanuni za Kielektroniki na Mawasiliano ya Posta GN No.61/2018 kuhusu kumlinda mlaji inayotaka mlaji kupewa taarifa kwa usahihi ya matumizi ya huduma muda wote, yanakiuka Sheria ya Ushindani namba 8/2003 inayotaka mtoa huduma kutoa huduma kwa kuzingatia zaidi maslahi ya watu wa hali ya chini, na sheria nyingine nyingi zimekiukwa.

Na tuelewane vizuri hapa, hakuna kitu kinaitwa VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA. Sheria iko wazi kuwa neno,maneno,sentensi au msemo wowote wenye lengo la kusigina haki ya mtu/watu ni batili.

Basi nitaviomba vyombo vya maamuzi vitusaidie kuyaweka sawa haya matano.Tutazidi kupeana taarifa kadri inavyokwenda.

Someni Hiyo Baada Ya Game Kuna Point Za Msingi Hapo
 
Big up mkuu. Ni kama vile ulikuwa kwenye akili yangu. Huwa napata tabu sana na hii kitu haya makampuni wanaita kifurushi "kime-expire" na hayo madudu mengine, yaani ni ujambazi mtupu(sio hata wizi tena). Jamaa ni washenzi sana. Wanakera sana!!!
 
Halotel ni ashushushu toka vietnam, wanajua kuiba na mitambo ya TCRA wameshindwa kunasa, hii nchi ni shamba la bibi
Duuu, kumbe wametuzid uwezo na tcra hawawez kuwachukulia hatua mana hawatakuwa na ushahid
 
Ukifungua hiyo kesi yako unadondokea pua kabla hata haijafika kwa hakimu,yaani unadondoshwa kwenye level ya ushauri wa mwanasheria tu au unadondokea pua kwenye korido za TCRA.
Wewe ni mtu dhaifu sana na kipindi cha NYERERE watu hovyo kama wewe ndio walichelewesha uhuru.
Watoto wa kike , ambao wakati wa kutita wanachuchumaa wanakuzidi ujasiri, woga wako ndio umaskini wako.
 
Habari wakuu.

Niende kwenye mada ni kwamba hili suala la ukomo wa vifurushi vya mitandao ya simu unapojiunga limekaaje?

Hivi ni haki mtu akijiunga apangiwe muda wa ku-expire kwa kifurushi?

Mfano nimeuziwa kifurushi kwa shilingi 1,000 halafu nikapewa mathalan dakika 20,SMS 100 na MB 100 kwa saa 24 halafu nikatumia dakika 10 pekee let say ambazo gharama yake ni shilingi 300 kati ya shilingi 1,000 niliyonunua kifurushi sasa muda unapoisha hiyo 700 wanayoichukua sio kitendo cha wizi?

Mfano umeniuzia bidhaa kwa shilingi 1,000 na nikakulipa kikamilifu iweje unipangie muda wa matumizi wakati nimeshakulipa pesa yako kikamilifu?

Hivi serikali haioni wizi wa mchana kweupe wanaofanyiwa wananchi wake kupitia mitandao hii ya simu? Nchi nyingi zimeachana na vitendo hivi vya wizi vyakumpangia mlaji muda wa kutumia bidhaa yake aliyoilipia kihalali nadhani bado sisi ndo tunaendelea kuibiwa na mitandao ya simu.

Kwanini wasijifunze kwa wenzao wa Tanesco ambapo wakikuuzia unit za LUKU hawakupangii ukomo wa muda wa matumizi badala yake utatumia unit zako hadi zitakapokwisa.

Unakuta wakati mwingine umejiunga kifurushi halafu mtandao wao ukasumbua kutwa nzima unakuja kushtuka kifurushi chako kimekwisha bila kukitumia na wala hawakufidii salio lako.

Au mwinhine amejiunga halafu umeme ukakatika hivyo kutokutumia kifurushi chake au mwingine alikuwa bize tu hajatumia kifurushi chake anashtuka anaambiwa muda wa kutumia kifurushi umeisha.

Yapo mengi yanayofanywa na mitandao ya simu kinyume na sheria ntaendelea kuyaorodhesha angalau watuhurumie kwa muda ambao wametupiga inatosha.

Serikali yetu sikivu tunaomba mlifanyie kazi hili kwa maslahi ya wanyonge ambao kuipata shilingi mia tano kwao ni mtihani mkubwa halafu bado akijiunga anapangiwa ukomo wa kutumia kifurushi chake ambacho amekinunua hivyo kuwa mali yake.

Pia mitandao ya simu iruhusu kugawa baadhi ya dakika, sms ama data kwa mteja mwingine ndani ya mtandao husika. Mfano mimi nimejiunga nimepata dakika, SMS na data lakini kuna mtu hana salio kabisa basi iwe ni kawaida kupunguziana dakika, meseji ama data.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom