Bashiru Ally kuondolewa ikulu kama katibu kiongozi kunatupa picha gani? Wahafidhina hawakufurahia uteuzi wake?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Hii sio kawaida kabisa katibu mkuu kiongozi kuhudumu kwa muda wa mwezi mmoja tu.

Japokuwa aliyemteua aliaga dunia kwa mapenzi ya Mungu hii sio kawaida, ni sawa na mtu alikuwa anaviziwa itokee bahati mbaya ili avurumishwe nje.

Katibu mkuu kiongozi ni nafasi nyeti na kubwa sana hapa nchini. Mtu kuitumikia kwa mwezi mmoja kisha akaandoshwa kuwa hafai sio jambo la kawaida.

Je, wahafidhina wa chama tawala walikuwa hawamtaki? Ila aliyemteua alilazimisha.
 
Hii sio kawaida kabisa katibu mkuu kiongozi kuhudumu kwa muda wa mwezi mmoja tu.

Je, wahafidhina wa chama tawala walikuwa hawamtaki? Ila aliyemteua alilazimisha.
Hapo chini ndipo kwenye jibu sahihi. Na binafsi naungana na hao Wahafidhina! Maana vyeo vya kiutumishi na kitaalamu, vilichezewa sana kwenye utawala wa Hayati!

Haiwezekani Mtu ameshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni, anazawadiwa Ukurugenzi wa Halmashauri! Huku wakuu wa idara waking'azang'aza tu macho.
 
Dr. Bashiru ni kada wa CCM sasa angeweza vipi kusimamia maadili na nidhamu ktk utumishi wa umma?

Uteuzi wa Dr. Bashiru ulifanywa na kiongozi mbabe asiyeheshimu sheria na taratibu.

Rais Samia Hassan ametambua kasoro ktk uteuzi huo na ndio maana ameutengua.
 
Hapo chini ndipo kwenye jibu sahihi. Na binafsi naungana na hao Wahafidhina! Maana vyeo vya kiutumishi na kitaalamu, vilichezewa sana kwenye utawala wa Hayati!

Haiwezekani Mtu ameshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni, anazawadiwa Ukurugenzi wa Halmashauri! Huku wakuu wa idara waking'azang'aza tu macho.
Haaaa, wewe na wahafidhina mna mambo.
 
Back
Top Bottom