MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hatimaye fursa imekuja mlangoni kabisa mwa makazi ya Ufipa. Huyu katibu mkuu wa zamani atawafaa sana Ufipa kuwa mgombea wao wa urais endapo atajitoa au kufukuzwa CCM kufuatia hili sakata lake linaloendelea. Mimi kama mtu ninayependa kuona upinzani unastawi basi ninawasihi ndugu zangu kwa kipindi hiki muendelee hivyohivyo kumtetea Bashiru ili siku akiachia ngazi iwe rahisi kwenu kumwomba awe mgombea wenu wa urais 2025.
Baada ya Ndugai kuachia uspika niliona pia angefaa kusajiliwa na Ufipa kuwa mgombea wao ila bado Spika mstaafu ana mapenzi sana na CCM hivyo uwezekano wa kuhamia Ufipa ni mgumu. Mzee Badhiru atawafaa kwa sababu pia alikuwa mpinzani kwa muda mrefu.
Ikishindikana kwa hao wawili basi subirini 2025 kwasababu kuna makada wa CCM wasio na subira watasusa na kutimkia upinzani baada ya majina yao kutopitishwa kugombea. Pale mtapata mgombea urais bila shida.