Ameongeza kuwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi ni chombo cha kisera kinachotumika kujinadi kama chama, kuomba kukubalika kisiasa, na kuhakikisha kabisa kwamba ilani hiyo inaleta mabadiliko katika maisha ya watu, na kuwa CCM ikekuwa ikiaminika kwa muda mrefu kutokana na sera zake.
"Nadhani kwa muda mrefu, chama kimeaminika kutokana na kuuza hiyo sera na kuitekeleza. Lakini, kama ilivyo taasisi yoyote, si chama kilichokamilika. Ni taasisi ambayo inaendelea kubadilika, inaendelea kukosolewa, na inaendelea kujisahihisha kama kilivyo chama chochote cha siasa mahala popote duniani.
Chama chochote cha siasa hakiwezi kuepuka makosa, hakiwezi kukosa udhaifu, lakini kwa kiwango kikubwa ni chama ambacho bado kimebeba matumaini ya Watanzania walio wengi. Ni chama ambacho bado kinaaminika na Watanzania walio wengi, lakini chama ambacho kinalazimika kujiboresha na kujisahihisha kadri jamii inavyobadilika."- Amesema Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Ally, kwenye mahojiano yaliyorushwa na Nijuze