The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Kuhusu kutenda haki kwa wagombea wote, Dkt. Bashiru amesema:
”Nadhani kama umemsikiliza Mwenyekiti wetu jana wakati anaapisha baadhi ya viongozi, alisema yeye kama mwenyekiti wa chama hana mgombea, na akaenda mbali kusema Makamu wa Rais, hana mgomnea; akamtaja Waziri Mkuu, hana mgombea; akamtaja Makamu Mwenyekiti, Mzee Mangula, hana mgombea; akanitaja mimi, sina mgombea.”
“Matarajio yetu, viongozi wanaokaa kwenye vikao vya uteuzi wana dhamana kubwa ya kutenda haki kwa wagombea wote. Hata kama ni mkeo, hata kama ni mwanao, hata kama ni rafiki yako mulisoma wote, hata kanma ni tajiri yako kakuajiri – unalinda maslahi ya chama siyo maslahi ya mgombea. Na kwahiyo upo upande wa chama, si upande wa wagombea”
Kuhusu wanaoachia nafasi zao na kuusaka ubunge, Dkt. Bashiru amesema:
"Na ndiyo maana hairuhusiwi mtu anayegombea kushiriki katika vikao. Naomba nitaje jambo ningependa mtusaidie. Kuna baadhi ya wenyeviti wetu wa mikoa; sasa hivi wamefikia watatu -- mikoa mitatu. Wanaopaswa kukaa kwenye vikao vya kamati za siasa za mkoa (ndiyo wenyeviti); Kamati ya Usalama na Maadili (ndiyo wenyeviti); Halmashauri Kuu ya Mkoa (ndiyo wenyeviti). Sasa wameamua wao waache kiti wajadiliwe badala ya kuwajadili wengine. Na wakati wanaomba uongozi walikabidhiwa dhamana ya kusimika uongozi madhubuti wa kukiletea chama ushindi. Sasa wamaemua kuingia kwenye foleni ya kujadiliwa."
Kanuni yetu inasema:
Mwanachama atakuwa na haki ya kugombea nfasi yoyote ya uongozi lakini edapo kugombea nafasi nyingi kutasababisha kuzorota kwa uhai wa chama, hatateuliwa.
"Una haki ya kugombea lakini vikao vikisema wewe unafaa zaidi kuwa mwenyekiti, na ukitoka kwenye uenyekiti mkoa utayumba, sasa unafaa uenyekiti kuliko ubunge, unaweza ukaambiwa kaa kwenye uenyekiti kwa maslahi ya chama na uhai wa chama. Na wanajua hayo hao viongozi wetu."
“Ukishakuwa kiongozi hutakiwi kuwa na tamaa, ndiyo ujumbe Mwenyekiti ametuambia. Unatakiwa kutosheka, na ni moja ya sifa za kiongozi. Tosheka na dhamana uliyopewa na ukamilishe hiyo dhamana, upimwe kwadhamana hiyo – siyo unatangatanga tu.”
“Ni haki yake, ni haki yake; lakini ajue angepimwa vizuri kwa ngazi yake ya ukuu wa Mkoa. Najua baadhi ya wakuu wa mikoa ambao wamekaa kwa muda mrefu na majina yale utafikiri ni cheo yale. Nsa Kaisi watu wengine wangedhani kuna cheo kinaitwa Nsa Kaisi, lakini kwa kwasababu amekaa kwenye nafasi ile na ameitumikia kama Mkuu wa Mkoa.”
“Kuna mtu unakuta ndani ya miaka mitano tu kapata vyeo vikubwa viwili kwa mpigo alafu kabla hajakomaa pale, anataka ubunge. Ni haki yake lakini ni vizuri kujitathmini na kujitafakari.”
Msimamo wake wa kutogomea nafasi yoyote
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dr. Bashiru Ally Kakurwa ameweka wazi msimamo wake wa kutogombea nafasi yoyote katika Chama hicho kwani ameridhika na nafasi aliyonayo.
“Mimi sigombei na siwezi kugombea, nimeshakuwa Katibu Kuu nagombea cheo gani?, cheo gani cha maana kuliko kazi hii ya kusimamia haki katika Chama” Katibu Mkuu CCM, Dkt.Bashiru
“Ukishakuwa kiongozi hutakiwi kuwa na tamaa ndio ujumbe Mwenyekiti ametuambia, unatakiwa kutosheka ndio moja ya sifa za kiongozi, tosheka na dhamana uliyopewa na uikamilishe hiyo dhamana na upimwe kwa dhamana hiyo sio unatangatanga tu” Dkt. Bashiru Ally