Bashiru una akili zaidi ya unavyoonyesha hadharani

Bashiru ....anapigania tumbo na Magufuli anapigania tumbo , siasa ndani ya ccm ni wizi mtupu ,


Mimi mjomba wangu kaishia darasa la V!! Ni katibu wa Uvccm hapo kemondo alipokuwa Bashiru anauza samaki, sasa wanamtumia kama karai kila uchaguzi ila awampi hata Shamba la mihogo kabaki kuwa karai.
 
Nyerere alikuwa akiendaga pale Nkrumah hall Udsm kufanya mijadala na wanataaluma, sasa huyu Bushiri hebu aige utaratibu huo na amshauri mwenyekiti wake pia aigilizie utamaduni huo wa kufanya mijadala na wasomi.
Mwwnyekiti wake atakachoishia kufanya ni kufoka foka tu kama Kenge.
 
Lissu yuko sahihi kabisa, Bashiru ame 'assimilate' na mfumo wa CCM, kwenye system inayo adhibu wenye uthubutu na maarifa basi wajinga ndio wanaoshamiri, sasa kwakua Bashiru analinda ugali wake ni lazima ajifanye mjinga siku ipite.
Hahaaaa....... Politics zinaondoa kabisa utimamu wa akili... ..... Lkn mtu mmoja tu Tundu Lissu hajawahi kutetereka kwenye kusimamia haki na raslimali za nchi....
 
Yaani umeandika point moja kubwa na ya msingi sn na ambayo ndio ukweli halisi👇👇

Na hii inafanya kufikiri kuwa Form six failure akiwa Chedema anaufahamu mkubwa kuliko Prof. aliyekuwa CCM.
 
Ccm wanakutumia km toilet paper wanakuacha..... Mifano ipo mingi sn
 
Maccm yajitafakari..... Hii tabia ya kua km misukule hailisaidii taifa hili
 
Majibu yako haya yanashikiliwa na utafiti upi ulioufanya? Kama kweli unaongozwa kwa akili yako kuandika hivi, utakuwa mnafiki wa kiwango Cha juu Sana! Nani asiyejua na hakumsikia sumaye kipindi like akiwa waziri mkuu akisema kuwa, " ulitaka Mambo yako yaende sawasawa Basi Hina budi kuwa ccm"!
Matajiri hawajiungi ccm kwa utashi wao Bali wanajisalimisha ili Mambo yao yanyooke! Wasomi halikadhalika wanataka vyeo, madaraja na maslahi! Na ccm imekuwa ikiwatishia na hata kupora au kufilisi Mali za matajiri waliokaidi kujiunga au kuunga juhudi! Haya yapo wazi Sana na Wala usiwalaumu wanachama wa vyama vingine kwa kuwa na mtazamo wako usio na ushahidi wa kitafiti! Ni kweli na haki kusema kuwa Sera ya ccm ni kuwa na wanachama wajinga wengi ambao imewaandaa kwa miaka mingi ili uendelee kuwatumia kutawala! Angalia mifumo ya elimu na aina ya elimu katika taasisi mbalimbali usivyo na maana ya kumkomboa aliyeipata!
Ukweli lazima usemwe ili mbadilike!
 
Phd wengi wa bongo ni mzigo kwa taifa
Mabadiliko ya nchi hii hayataletwa na wasomi wa PhD. Yateletwa na watu wa kitaani - ambao kwangu ndio mashujaa wangu. Katika mfumo huu chovu ambamo rais nu mungu-mtu, maPhd wamechukua mkondo wa kijipendekeza kwa watawala ili waendelee kuajiriwa na kuteuliwa, wanaangalia maslahi binafsi. Watu wakitaani hawana cha kupoteza na ndio askari wetu wa mstari wa mbele kuelekea kupata uhuru wa kweli, haki na maendeleo ya watu. Binafsi ninawapongeza askari hawa.
 
Ccm inatakiwa kuendelea kutengeneza tabaka la watu wasio na chakupoteza. Hawa watu ni muhimu sana kwa mabadiliko ya kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…