Bashungwa aendeshaje home affairs, ili hatimaye taifa likae katika Utulivu na amani, wasiwasi uwaondoke Watanznaia

Bashungwa aendeshaje home affairs, ili hatimaye taifa likae katika Utulivu na amani, wasiwasi uwaondoke Watanznaia

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Mimi binafsi ningemshauri, aifanye polisi isimame kama chombo huru kinachofanya mambo yake kwa mujibu wa kanuni ambazo zipo, na kisiwe chombo ambacho kinapokea maagizo kutoka taasisi zingine za kiusalama mfano tiss kuipa kazi polisi, pengine jukumu lilipaswa kushughulikiwa na tiss wenyewe!,

Polisi izingatie mipaka yake ya kiutendaji, kuchunguza, kupeleleza, kukamata, na kupeleka mahakamani,
Magereza jeshi, ni jeshi lisilovuka mipaka yake ya kikazi, basi na taasisi zote za kiusalama, kuwa na utii wa kuheshimu mipaka yao ya kikazi,

#-Tumsaidie juu ya kipi Kifanyike ili kuondosha woga, na tafarani zilizopo na zinaziendelea, ambazo zingine zimeanza kusababisha majanga!
 
Si tuliambiwa kuna vikosi nje ya vikosi, je ana ubavu wa kushughulika na 'wenye ubavu'?
 
Si tuliambiwa kuna vikosi nje ya vikosi, je ana ubavu wa kushughulika na 'wenye ubavu'?
Vikosi vya kiulinzi na usalama vyote visimame ndani ya mstari wao wa kimajukumu,
Vikosi vya mifukoni ndivyo vinavyoharibia kazi Vikosi ambavyo Vipo kitaaluma na kimfumo wa kikatiba, pia ndivyo vinavyotumika katika, chuki, visasi na ya hovyo hovyo, ipo haja ya kurudi kwenye mistari ya kiutendaji kazi kwa mujibu wa sheria na katiba.
 
Mawaziri hawana uwezo wowote wa kupinga chochote, Nchi hii haiendeshwi kwa yaliyoandikwa kwenye Katiba, Inaendeshwa na kikundi cha watu fulani kwa katiba za mfukoni
Nchi hii haiendeshwi kwa yaliyoandikwa kwenye Katiba, Inaendeshwa na kikundi cha watu fulani kwa katiba za mfukoni📌🔨
 
Mawaziri hawana uwezo wowote wa kupinga chochote, Nchi hii haiendeshwi kwa yaliyoandikwa kwenye Katiba, Inaendeshwa na kikundi cha watu fulani kwa katiba za mfukoni
Upo sahii , tusitegemee mabadiliko , shida ya nchi hii kila mtu anafika mahala kwa sababu mtu mmoja tu ndo ametaka , sasa utawezaje kutenda tofauti , katiba mpya ni lazima.

Watu wanafaya kazi kwa kuogopa maana anaweza amuka hasubui mkeka umechanika, ni shida sana
 
Inno yeye sio maneno mengi ni vitendo dhidi ya maneno, Mafwele na Wambura pamoja na Murilo wapashe misuli mda wowote wanahamishiwa maporini huko
 
Mimi binafsi ningemshauri, aifanye polisi isimame kama chombo huru kinachofanya mambo yake kwa mujibu wa kanuni ambazo zipo, na kisiwe chombo ambacho kinapokea maagizo kutoka taasisi zingine za kiusalama mfano tiss kuipa kazi polisi, pengine jukumu lilipaswa kushughulikiwa na tiss wenyewe!,

Polisi izingatie mipaka yake ya kiutendaji, kuchunguza, kupeleleza, kukamata, na kupeleka mahakamani,
Magereza jeshi, ni jeshi lisilovuka mipaka yake ya kikazi, basi na taasisi zote za kiusalama, kuwa na utii wa kuheshimu mipaka yao ya kikazi,

#-Tumsaidie juu ya kipi Kifanyike ili kuondosha woga, na tafarani zilizopo na zinaziendelea, ambazo zingine zimeanza kusababisha majanga!
Tatizo ni CCM kusimama kama mtawala, mwingereza alisimama kama msimamizi wa Tanganyika akipokea amri toka UNO, kutokana na hilo hakuweza kufanya kama alivyofanya Kenya alikokuwa mtawala. CCM baada ya viongozi wake kutajirika wamelazimika wajijengee ukuta wa kujilinda dhidi ya wananchi waliogeuzwa kuwa watawaliwa, kutokana na hilo, polisi wamepewa jukumu la kuulinda ukuta kwa kila namna wawezayo, na wakulibadilisha hilo ni viongozi wa CCM na si mwingine.
 
Back
Top Bottom