PreGE2025 Bashungwa alishukuru Bunge kwa kupambana na watu wa nje wasioitakia mema nchi

PreGE2025 Bashungwa alishukuru Bunge kwa kupambana na watu wa nje wasioitakia mema nchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014

Waziri wa Mambo ya Ndani, Innocent Bashungwa amemshukuru Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Tulia Ackson kwa kuwa Bunge lake limesimama na Serikali dhidi ya watu kutoka nje ya nchi wasiokuwa na nia njema na nchi.

Bashungwa amesema hayo leo Juni 9, 2025 wakati akimkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe a kufunga mafunzo ya maofisa na wakaguzi wa Jeshi la Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

“Tumeshuhudia Bunge likisimama na Serikali kindakindaki pale masilahi ya Taifa letu yanapoguswa. Hata pale watu kutoka nje ya nchi wasioitakia mema nchi yetu, tumeshuhudia Bunge letu likitetea heshima ya nchi yetu,” amesema.

Kauli ya Bashungwa imekuja kufuatia michango ya baadhi ya wabunge waliokuwa wakichangia katika Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani Mei 26 na 27, 2025 wakikosoa wanaharakati kutoka Kenya na Uganda waliokuja nchini kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu lakini walirejeshwa katika nchi zao.

Hata hivyo, Dk Tulia alijitenga na kauli za wabunge hao akisema sio msimamo wa Bunge.

Soma hapa Spika Tulia ajitenga na kauli za Wabunge
 
Back
Top Bottom