Bashungwa Awabana Wataalam na Mkandarasi SITE, "Naweza Kufukuza Timu Yote"

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

BASHUNGWA AWABANA WATAALAM NA MKANDARASI SITE, "NAWEZA KUFUKUZA TIMU YOTE"

Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema hatasita kubadilisha timu ya Wataalam na Mkandarasi wanaoendelea na kazi ya kurejesha mawasiliano ya barabara ya Dar es salaam- Lindi katika eneo la Nangurukuru kutokana na kasi ndogo ya kazi na usimamizi.

Bashungwa ameonesha hali hiyo ya kutoridhishwa na usimamizi na kasi ya urejeshaji wa mawasiliano katika eneo hilo na kumtaka Mtaalamu na Mkandarasi kuongeza kasi ili wamalize zoezi ndani ya muda uliotolewa.

"Mimi naweza kufukuza timu yote, bora niwaambie watanzania timu hii imefeli na niagize nyingine ambayo inaweza ikaja kufanya kazi, hatuwezi kwenda hivi", amesema Bashungwa

Aidha, Bashungwa amemuagiza Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara TANROADS kutafuta na kuongeza magari ya kubeba mawe na vifusi pamoja na mitambo ili kazi ifanyilke usiku na mchana bila kusimama.
 
Baada ya kusikia nauli ya kutoka Dar kwenda Lindi kupitia Songea ni laki na 20 nilijua hii barabara ndo basi tena maana wenye mabasi watanogewa
 
Back
Top Bottom