Bashungwa: Tozo zimejenga vituo vya afya 234

Bashungwa: Tozo zimejenga vituo vya afya 234

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa amesema Serikali imejenga vituo vya afya 234 kutokana na fedha za tozo ya miamala ya simu ndani ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Bashungwa ameyasema hayo leo Septemba Mosi wakati akizungumzia manufaa ya tozo hizo ambazo zimekuwa zikipingwa na wadau mbalimbali kwa sababu tofauti ikiwemo kutozwa mara mbili au zaidi.

Amesema hadi kufikia Desemba 2020, Serikali ilikuwa imejenga hospitali za wilaya 102, vituo vya afya 487 na zahanati 1,198.

Amesema serikali ilifanya tathmini ya hali ya hospitali hizo na kuja na mradi wa kujenga vituo vya afya kwenye kila tarafa.

Amesema katika tarafa 570, tayari serikali imejenga vituo vya afya 234 kwenye tarafa 207 ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye aliingia madarakani Machi 19, 2021 baada ya kifo cha mtangulizi wake, Hayati John Magufuli.

“Kupitia tozo za miamala ya simu, tumeweza kujenga vituo vya afya 234 kwa Sh117 bilioni kwenye hizi tarafa 207 na kila kituo cha afya kimetugharimu Sh500 milioni.
“Ukiangalia toka nchi yetu imepata uhuru na awamu zote zilizotangulia, kuweza kujenga vituo vya afya 234 ndani ya mwaka mmoja, si jambo la kawaida,” amesema Bashungwa.

Amesema kinachopatikana kutoka kwenye kodi jumuishi, kinakwenda kutibu kiu ya wananchi ya kupata huduma za msingi kama vile afya, elimu na barabara na inasaidia kupunguza pengo kati ya wenye nanchi na wasio nacho.

“Tutaendelea kuhakikisha kwamba tunazitumia fedha hizi kutoa huduma bora za afya ya msingi katika maeneo mbalimbali nchini,” amesisitiza Bashungwa.

Kwa upande wa sekta ya elimu, amesema kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwamba, serikali inatakiwa kuendelea kujenga madarasa 15,000 kila mwaka ili kukidhi mahitaji hayo.

“Tathmini ambayo tumeifanya tunahutaji kuendelea kujenga madarasa yasiyopungua 15,000 kila mwaka hadi hawa waliopo kidato cha kwanza watakapoingia kidato cha sita, niwaombe Watanzania hii nchi ni ya kwetu tuendelee kuipa ushirikiano Serikali,” amesema Bashungwa.

Chanzo: Mwananchi
Nchi letu limekuwa la kipumbavu tangu akivyofariki JPM. Pamoja na kwamba mzee Naye alikuwa mnoko lakini kuna mambo alikuwa vizuri kuliko hizi takataka zingine! Ujenzi wote huo wanasema ni za tozo wakati kulikuwa na US$ 1.3m kutoka WB! Pia kulikuwa na pesa ya uviko 19, wasitufanye sisi ni mataahira! Pumbavu kabisa!
 
Walio na Phd ndani ya ccm ni wale wenye diploma kule chadema.
 
Wanatutia hasira tu!
Mfumo uliopo Tanzania ni viongozi 10 wa ccm waliopo kwenye nafasi za juu serikalini na ndani ya chama, hao wanawamiliki watu milion zaidi 50 wasio na uelewa na walio 10 senior staffs wanadai wana wanachama wengi kumbe wale walio wanachama ni wachumia tumbo.
Tukitaka kufanikiwa Tanzania na tutoke kwenye umaskini mkubwa
1. MaRc, madc na maded wapigiwe kura na wananchi kama wabunge
Hapa kutakuwepo na nidhamu na uwajibikaji mkubwa. Kwa sasa voongozi hao ni makada wa chama.
2. Nafadi ya IGP itangazwe na watu waombe.
3. Mawaziri kabla hawajaapishwa wapigiwe kura na wabunge .
3. Jaji mkuu wafanyiwe usaili kupatiksna kwao.
4. Wakurugenzi wa bodi na wenyeviti waombe kazi hizo na wafanyiwe usaili.
5. Habari ya muungano tuwe na serikali tatu ili tiheshimiane kila mtu atawale kwake.
6. Habari ya jinsua 50/50 watu wakutane kwenye usaili na sio kugawana nafasi muhimu kisingizio 50/50
7. Ubunge viti maalum wapigiwe kura kama walivyo wabunge wengine
8. Kuweo na nafasi za wagombea binafsi kwa nafasi za udiwani,ubunge na urais
 
Kwani huko vijijini ndio wanataka kukatwa hiyo tozo?
Ndio maana inawasaidia wao maana na mimi Niko kijijini..

Mnadekezwa Sana awamu hii, Mwendazake angekuwepo hapa hakuna mdomo mungenyanyua maana pesa mliporwa na mliufyata.
 
Mfumo uliopo Tanzania ni viongozi 10 wa ccm waliopo kwenye nafasi za juu serikalini na ndani ya chama, hao wanawamiliki watu milion zaidi 50 wasio na uelewa na walio 10 senior staffs wanadai wana wanachama wengi kumbe wale walio wanachama ni wachumia tumbo.
Tukitaka kufanikiwa Tanzania na tutoke kwenye umaskini mkubwa
1. MaRc, madc na maded wapigiwe kura na wananchi kama wabunge
Hapa kutakuwepo na nidhamu na uwajibikaji mkubwa. Kwa sasa voongozi hao ni makada wa chama.
2. Nafadi ya IGP itangazwe na watu waombe.
3. Mawaziri kabla hawajaapishwa wapigiwe kura na wabunge .
3. Jaji mkuu wafanyiwe usaili kupatiksna kwao.
4. Wakurugenzi wa bodi na wenyeviti waombe kazi hizo na wafanyiwe usaili.
5. Habari ya muungano tuwe na serikali tatu ili tiheshimiane kila mtu atawale kwake.
6. Habari ya jinsua 50/50 watu wakutane kwenye usaili na sio kugawana nafasi muhimu kisingizio 50/50
7. Ubunge viti maalum wapigiwe kura kama walivyo wabunge wengine
8. Kuweo na nafasi za wagombea binafsi kwa nafasi za udiwani,ubunge na urais
Hivi nikiwa kama mwanaccm nitakitetea vipi chama chama changu kama mambo yenyewe ndo haya ambayo hata asiye na akili anaelewa kuwa ni wizi wa mchana.
Yaani tunaomba mikopo kwa ajili ya Madarasa na Mahospital ndani ya mwaka mmoja then inaingia tena Tozo kwa ajili ya kujenga hichohicho kilichochukuliwa mkopo.
Tuseme wizi unafanyika mpaka mnasahau namna ya kuiba.
Hii ni hatari kubwa sana kwa kweli sasa hivi upinzani unanihusu siwezi kuongozwa na mijizi isiyokuwa na kumbukumbu.
Ila Mungu anayaona mnayotufanyia
 
Wakati huo samia alikuwa makamu wa Rais sada ni Rais.
2. Philip mpango alikuwa waziri wa fedha na mipango sasa ni makamu wa Rais.
3. Kasmim majaliwa alikuwa waziri mkuu bado ni waziri mkuu,
4.Mwigulu nchemba alikuwawaziri wa sheria na katiba sasa ni waziri wa fedha na mipango.
Kwa mantiki hiyo walihudika kuwadanganya wananchi na bado hadi sasa wataendeleza mbinu hiyo hiyo kuendelea kuwafanganya wanyonge ili waendelee kuwanyonyana kuwapa kura ili waendelee kuwapumbaza wanyonge?

Hao uliowataja ni products za Magufuli, hivyo ni lazima watumie uongo ule ule, maana wamejiaminisha kuwa Magufuli alipendwa kwa zile propaganda zake.
 
Back
Top Bottom