Bashungwa: Uwekezaji katika bandari una manufaa makubwa kiuchumi

Bashungwa: Uwekezaji katika bandari una manufaa makubwa kiuchumi

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
UWEKEZAJI KATIKA BANDARI UNA MANUFAA MAKUBWA KIUCHUMI: BASHUNGWA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambeye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa amesema maamuzi ya Serikali kuhusu Uwekezaji na uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam utaongeza ufanisi kiutendaji na manufaa kiuchumi wa nchi kwa kuongeza Mapato.

Ameeleza hayo wakati wa mwendelezo wa ziara yake jimboni ya Kuongea na Wananchi na kukagua miradi ya maendeleo katika Kata za Chonyonyo, Chanika, Rugera na Kihanga wilayani Karagwe.

“Tanzania tuna bandari ambayo ufanisi wake ulikuwa mdogo katika uendeshaji, ndio maana serikali ikaamua kutafuta mwekezaji ambaye ataongeza ufanisi ili tuweze kupata mapato zaidi ambayo yataenda kutoa huduma za kijamii kwa Watanzania” amesema Bashungwa

Bashungwa amewatoa hofu Wananchi wa Mkoa Kagera kwa kueleza kuwa bandari ya haiuzwi wala haibinafishwi bali Serikali inaleta mwekezaji ambaye ataendesha bandari hiyo kwa makubaliano yatakayoongeza ufanisi kiutendaji.

“Ndugu zangu Wananchi naomba tuyapuuze yanayosemwa huko mitandaoni, katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi tuliahidi kutengeneza ajira milioni nane ndio maana tumeamua kukaribisha uwekezaji utakaozalisha ajira kwa Watanzania”

Aidha, Bashungwa amesema Uwekezaji ni moja ya mkakati wa kupanua wigo wa vyanzo vya mapato ili Kondoa usumbufu kwa Wananchi kwa kutoweza tozo nyingi ambazo zingelitumika kutekeleza miradi mbalimbali nchini.

 
Sawa, ila at what cost? Tunaomba hoja zijibiwe...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Nani mwenye akili timamu aliyetegemea yeyote toka huko chamani kwao atoe maoni tofauti na Samia msaliti public?
 
UWEKEZAJI KATIKA BANDARI UNA MANUFAA MAKUBWA KIUCHUMI: BASHUNGWA

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ambeye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa amesema maamuzi ya Serikali kuhusu Uwekezaji na uendeshaji wa bandari ya Dar es Salaam utaongeza ufanisi kiutendaji na manufaa kiuchumi wa nchi kwa kuongeza Mapato.
Tutazame uhuni wa huko nyuma
Loliondo inatusaidia nini hivi sasa, Gas Mtwara na mikataba ya kishenzi ya mkwere inatusaidia nini hivi sasa
 
Hawa wacongo wasijifanye wanaijua Tanganyika kuliko WaTanganyika wenyewe… Endeleeni kujificha kwenye hili pipa tupu iko siku sijui akina basunga bashungwa halisi watasema kwao wapi
 
Kuna mtu anayepinga uwekezaje? Au anachepusha hoja?

Tena huyo ndiyo anyamaze kabisa.
 
CCM shida sana, yaani wako busy kutoa elimu huku wachonga deal wenyewe wametulia tu wakisubiri account kunona for life.
 
kwahiyo ni lazima siyo Watimize ilani yao bila kujali masilahi ya kitaifa kwa mikataba ya kipuuzi namna ile wakabidhi nchi kwa maharamia wenyewe wameshindwa
 
Back
Top Bottom