Bashungwa: Wataalam waliostaafu kuendelea kutumika katika ujenzi na matengenzo ya barabara

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
Wizara ya Ujenzi kupitia taasisi zake ERB na TANROADS inaandaa utaratibu wa kutumia wataalam wa ndani waliostaafu katika ujenzi na matengenezo ya barabara.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024

Amesema hatua hiyo ni katika kujenga uwezo wa ndani ya taasisi na wastaafu wabobezi katika usimamizi wa miradi badala ya kutegemea wataalam nje.

“Tumeanza utaratibu wa kutumia wataalam wa ndani waliostaafu yaani retired but not tired katika ujenzi na matengenezo ya barabara.”

Amesema Kitengo cha ndani cha Ushauri wa Kihandisi cha TANROADS (TECU) kinaendelea kuwatumia wahandisi wabobezi waliostaafu katika usanifu na usimamizi wa miradi.

“Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza utegemezi wa wahandisi washauri kutoka nje. Jambo hili la kutumia wastaafu pia linatoa fursa kwa wataalam wanaochipukia na ngazi ya kati kujifunza kutoka kwa wastaafu wabobezi ambao wako nyumbani wakati ujuzi wao bado unahitajika katika ujenzi wa taifa letu.”

Amesema TANROADS inatumia TECU katika usanifu na usimamizi wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja.

“Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za usimamizi wa miradi pamoja na muda unaotumiwa katika ununuzi wa wahandisi washauri.”

Amesema TECU imeshiriki kwa mafanikio katika utekelezaji wa miradi kadhaa ya kimkakati, ikiwemo Mradi wa Uzalishaji wa Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Njia 8 ya Kimara-Kibaha (km19.2), Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Geita, na ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri.

IMG-20240529-WA0480.jpg
 
Huyu Waziri naye huwa hata sielewi anataka nini?

Hivi huko nje huwa wanaenda kujifunza ni nini?

Tuna viongozi wa hovyo na wajinga haswa
 
Wizara ya Ujenzi kupitia taasisi zake ERB na TANROADS inaandaa utaratibu wa kutumia wataalam wa ndani waliostaafu katika ujenzi na matengenezo ya barabara.

Amesema Kitengo cha ndani cha Ushauri wa Kihandisi cha TANROADS (TECU) kinaendelea kuwatumia wahandisi wabobezi waliostaafu katika usanifu na usimamizi wa miradi.

“Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza utegemezi wa wahandisi washauri kutoka nje. Jambo hili la kutumia wastaafu pia linatoa fursa kwa wataalam wanaochipukia na ngazi ya kati kujifunza kutoka kwa wastaafu wabobezi ambao wako nyumbani wakati ujuzi wao bado unahitajika katika ujenzi wa taifa letu.”
Ina maana wahandisi nchini ni hao tu waliostaafu hakuna wengine waliokuwa chini yao, kwamba TANROADS hawaelewi hata maana ya succession plan? Tanzania kuna mambo mengine tunafanya kizembe kwa kiwango cha kushika rekodi ya dunia!

Waziri mzima unaongea mbele za watu utumbo kama huu, kwamba tusipotumia wahandisi waliostaafu tutaingia gharama za kutumia wahandisi kutoka nje? Ujinga sana huu.
 
Watu wanafukuzana na posho pekee hakuna la maana
 
Wizara ya Ujenzi kupitia taasisi zake ERB na TANROADS inaandaa utaratibu wa kutumia wataalam wa ndani waliostaafu katika ujenzi na matengenezo ya barabara.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa wakati wa kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2024/25, Bungeni jijini Dodoma leo, Mei 29, 2024

Amesema hatua hiyo ni katika kujenga uwezo wa ndani ya taasisi na wastaafu wabobezi katika usimamizi wa miradi badala ya kutegemea wataalam nje.

“Tumeanza utaratibu wa kutumia wataalam wa ndani waliostaafu yaani retired but not tired katika ujenzi na matengenezo ya barabara.”

Amesema Kitengo cha ndani cha Ushauri wa Kihandisi cha TANROADS (TECU) kinaendelea kuwatumia wahandisi wabobezi waliostaafu katika usanifu na usimamizi wa miradi.

“Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza utegemezi wa wahandisi washauri kutoka nje. Jambo hili la kutumia wastaafu pia linatoa fursa kwa wataalam wanaochipukia na ngazi ya kati kujifunza kutoka kwa wastaafu wabobezi ambao wako nyumbani wakati ujuzi wao bado unahitajika katika ujenzi wa taifa letu.”

Amesema TANROADS inatumia TECU katika usanifu na usimamizi wa miradi ya ujenzi wa barabara na madaraja.

“Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za usimamizi wa miradi pamoja na muda unaotumiwa katika ununuzi wa wahandisi washauri.”

Amesema TECU imeshiriki kwa mafanikio katika utekelezaji wa miradi kadhaa ya kimkakati, ikiwemo Mradi wa Uzalishaji wa Umeme wa Bwawa la Mwalimu Nyerere, Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Njia 8 ya Kimara-Kibaha (km19.2), Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Geita, na ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Mbigiri.

View attachment 3002999
Waajiri watu wako wengi tuu sio Tanzania pekee hata Nje ya Nchi wako Wabongo wanafanya kazi huko.

Badala ya Kuajiri waliostaafu waweke mzigo mezani Ili watu wajitokeze.

La sivyo semeni hamna pesa maana hata mapolisi wameajiri wale waliostaafu
 
Barabara njia 4 za kuingia na kutoka kwenye majiji yetu ni muhimu kuondoa congestion
 
Back
Top Bottom