Basi gani linalotoka Mbeya kwenda Masasi/Mtwara?

Basi gani linalotoka Mbeya kwenda Masasi/Mtwara?

Zekoddo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
1,859
Reaction score
4,539
Habari Wazee wenzangu,

Naulizia bus za kutoka Mbeya hadi Masasi au Mtwara Mkoani.

Kama zipo ni kampuni gani na nauli ni shilingi ngapi hadi Masasi Town.

Asante.
 
Nilikuwa nataka nifahamua na bei yake kabisa ili nijipange mazima nikitoka huku wilayani.. nikifika hapo Green City kesho yake niamshe mapema.
superfeo - mby to mtwara
superfeo - mby to masasi
Sajda - mby to Masasi
 
Nauli ni Tzs 55,000/=
Bus ziendao huko ni Super Feo na Sajda, hakuna nyingine tofauti na hizo
 
Super feo bus kubwa na vipisi huwa wanaenda Mbeya so wanapitia Makambako, Njombe, Madaba, Songea,Namtumbo, Tunduru, Nakapanya, mangaka, then masasi
 
Iling'olewa kumzuia MRENO....
Kweli kabisa,, miaka mingi sana Ile mikoa Haina reli Wala treni.. Ila mwaka huu Mama Samia kawaona,, wanapigiwa barabara ya treni ya umeme mpaka Ntwara😃
 
Mkuu hukusoma jiografia

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Mkuu Mambo ya mabus na nauli zake yanafananaje na jiografia ya nchi..?
Na Umri wangu huu nimebahatika kutembea zaidi ya Mikoa 10 na wilaya zake Tz hii,, bado unaniuliza mambo ya Jiografia kweli🤔🤔
 
Back
Top Bottom