Basi kampuni ya Mallesa lagongana uso kwa uso na lori, wawili wafariki dunia

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Watu wawili wamefariki dunia baada ya basi la Kampuni ya Mallesa walilokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mkoani Geita kugongana na lori la mizigo katika Kijiji cha Rumasa, Wilaya ya Chato mkoani Geita.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Safia Jongo, amezungumza na TBC Digital kwa njia ya simu na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema imetokea majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo, Oktoba 7, 2025.

Lori la mizigo lililogongana na basi hilo lilikuwa limebeba vifaa vya ujenzi na lilikuwa likisafiri kutoka mkoani Mwanza kuelekea wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
​
 
mmiliki wake anaitwa nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…