Basi kusiwe tena na Samia Scholarship

Basi kusiwe tena na Samia Scholarship

harunimaiga

Member
Joined
Nov 13, 2022
Posts
26
Reaction score
47
Serikali kuondoa utambuaji wa shule Bora na wanafunzi Bora kwa kisingizio wengi wao wanakua ni kutoka private schools sio sawa. Shule za advance za private wanaosoma pia Wana Hali nzuri za kimaisha na ndo pia wanafaulu kwa alama za juu zaidi.

Ili upate SAMIA scholarship lazima pia huwe na division 1 Kali ndo upate scholarship. Sasa ukiangalia wanaofaulu kwa alama za juu kidato cha sita wanatoka shule za private ambao tunaweza sema wana hali nzuri ya kiuchumi.

Hivyo basi hizi scholarship za Mama zinakua zinawatenga wanafunzi wengi walosoma shule za serikali,Kwan ufaulu wao sio mzuriiii ukilinganisha na wanafunzi wa shule binafsi.

Kwa sauti yangu ndogo, swala hili nalo lifikiliwe kama wameona jambo walilofanya ni sahihi. Kwani kwa Hali hii na masharti ya hii scholarship zitakuwa zinawanufaisha wale wenye hali nzuri kiuchumi na kuwaacha Hawa wengi wenye uchumi wa chino.

Au ndio Ile mwenye nacho uongezewa?
 
Elimu ya Tanzania inazidiwa na mtoto idi wa hapa bongo ambae anajua kusoma na kuandika tu
 
Scholarship ya mchongo. Unampa scholarship kwa kisingizio cha kuongeza rasimali watu, wakati rasimali watu waliopo hawaajiriwi, si wataalamu wa afya, si wahandisi, watu wapo kitaa mwaka wa tano huu.
 
Hizi ndio siasa chafu zinazoharibu elimu. Tutafute vichwa vitakavyolipeleka taifa mbele. Kigezo ni division one Kali na sio umaskini au utajiri.
 
Back
Top Bottom