Basi la Kagera sugar

Basi la Kagera sugar

Alubati

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2016
Posts
6,535
Reaction score
14,840
Hili basi linalobeba wachezaji wa timu ya soka ya Kagera sugar limepaki pembeni ya barabara ya Morogoro-Dodoma maeneo ya Kihonda kwa muda wa mwezi mmoja sasa.

Nadhani litakuwa na hitilafu, kwanini wasilipeleke kupaki gereji kwa kuvutwa au kupakiwa kenye yale magari maalum.

Hofu yangu lisije kuwa chanzo cha ajali kwa watumiaji wa barabara hiyo hasa nyakati za usiku.

Askari wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro hamlioni hili?.
Screenshot_20230705_091320_Facebook.jpg
 
Haa Lipo Sana Ila Limekaa Vema Linaweza Ondoka Muda Wowote
Limeharibika Kifaa Kikubwa Sana Hizo Tata Hata Dodoma Jiji Wanalo
 
Hili basi linalobeba wachezaji wa timu ya soka ya Kagera sugar limepaki pembeni ya barabara ya Morogoro-Dodoma maeneo ya Kihonda kwa muda wa mwezi mmoja sasa.

Nadhani litakuwa na hitilafu,kwanini wasilipeleke kupaki gereji kwa kuvutwa au kupakiwa kenye yale magari maalum.

Hofu yangu lisije kuwa chanzo cha ajali kwa watumiaji wa barabara hiyo hasa nyakati za usiku.

Askari wa usalama barabarani mkoa wa Morogoro hamlioni hili?.View attachment 2679285
Niambie liko wapi nikajichomolee vitu vya muhimu kwenye injini.
 
Muda huu naenda kihonda nipo nalipita daah
Nililiona Kwa Mkomola pale almost wiki mbili nyuma.

Ni kweli, limekaa sehemu si salama. Wangelivuta hata kuliacha pale Petrol Station walau.

Mamlaka zinasubiri kupewa amri ya Kuunda Tume ya Kuchunguza Ajali.
 
Mwezi mzima lipo hapo aisee... yes pale kituo cha mafuta kwa pembeni ni sehemu salama zaidi kwa kulipaki.
 
Timu kongwe hiyo haina hela ya kuvuta na kukarabati basi. Inaibuka timu kutoka singida ndani ya msimu mmoja ishapata hela ya kusajili hadi wabrazil na hakuna anayejali. Nchi hii ? Duh
 
Timu kongwe hiyo haina hela ya kuvuta na kukarabati basi. Inaibuka timu kutoka singida ndani ya msimu mmoja ishapata hela ya kusajili hadi wabrazil na hakuna anayejali. Nchi hii ? Duh
Kumanisha nini
 
Back
Top Bottom