Basi la klabu ya Simba SC,
Wekundu wa Msimbazi, ambalo lililokuwa limewabeba wanachama na mashabiki wa timu hiyo kutoka Tanzania, likielekea mjini Ndola, limepata ajali baada ya kugongana na Lori maeneo ya Kapiri Mposhi nchini Zambia.
Kwa taarifa za awali haikufahamika mara moja chanzo cha ajali hiyo huku mashabiki na wanachama wakiwa wapo salama hakuna aliyeumia zaidi ya uharibifu wa gari hilo.
Simba SC itaingia uwanja wa Kalampa Kitwe nchini Zambia Jumamosi Disemba 15, 2018 kucheza na Nkana FC katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
View attachment 968094