Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,199
Nimeshitushwa na habari hii kutoka katika gazeti la mwananchi la leo.
WATU 12 raia wa Ethiopia wamehukumiwa na mahakama ya Wilaya ya Singida, kulipa faini ya Sh100,000 kila mmoja baada ya kukiri makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya Tanzania bila ya kuwa na kibali halali.
Kwenye red, hii ni double standard. Ni kwa vipi basi lililobeba wahamiaji haramu linataifishwa ilihali meli ya kinana iliyobeba meno ya tembo kwenda Hong Kong haikutaifishwa? Hapo kosa kubwa na dogo ni lipi? Kwanini makosa yanayofanana yanatolewa hukumu tofauti? Au hukumu zinatolewa kwa utashi wa hakimu? Kwanini Kinana alipokiri kwa mdomo wake kwamba meli yake ilibeba pembe za ndovu kupeleka HongKong hakufunguliwa mashitaka na meli yake itaifishwe?Pia mahakama hiyo, imeamuru basi la Kampuni ya Mtei ya mjini Arusha lililokuwa limebeba Waethiopia hao kukamatwa na kutaifishwa kuwa mali ya Serikali.