Basi la Mtei lataifishwa kwa kubeba wahamiaji haramu

Basi la Mtei lataifishwa kwa kubeba wahamiaji haramu

Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
5,143
Reaction score
3,199
Nimeshitushwa na habari hii kutoka katika gazeti la mwananchi la leo.

WATU 12 raia wa Ethiopia wamehukumiwa na mahakama ya Wilaya ya Singida, kulipa faini ya Sh100,000 kila mmoja baada ya kukiri makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya Tanzania bila ya kuwa na kibali halali.
Pia mahakama hiyo, imeamuru basi la Kampuni ya Mtei ya mjini Arusha lililokuwa limebeba Waethiopia hao kukamatwa na kutaifishwa kuwa mali ya Serikali.
Kwenye red, hii ni double standard. Ni kwa vipi basi lililobeba wahamiaji haramu linataifishwa ilihali meli ya kinana iliyobeba meno ya tembo kwenda Hong Kong haikutaifishwa? Hapo kosa kubwa na dogo ni lipi? Kwanini makosa yanayofanana yanatolewa hukumu tofauti? Au hukumu zinatolewa kwa utashi wa hakimu? Kwanini Kinana alipokiri kwa mdomo wake kwamba meli yake ilibeba pembe za ndovu kupeleka HongKong hakufunguliwa mashitaka na meli yake itaifishwe?
 
Tofauti ni kuwa meli ni ya mtu wa chama chetu, wakati basi ni la mtu wa chama chenu.

Isije kuwa mmiliki wa basi hilo akawa yuleyule muasisisi wa chama kinachotusumbua usiku na mchana, hapo ndio tena basi!!!
 
Hii ni kali! Kwenye daladala sasa tutahitajia kuonyesha Pasi za Tanzania!
 
Hii ni kali! Kwenye daladala sasa tutahitajia kuonyesha Pasi za Tanzania!
Hicho ndiyo kinachonishangaza. Maana kwenye meli, kabla ya kupakia mzigo, unatakiwa ukaguliwe na mwenye meli ajiridhishe kwamba mzigo unaosafirishwa ni halali. Sasa kwenye basi, mwenye basi atajuaje kama abiria anayeingia au kukodi gari lake ni mtanzania au la? Na je kuna sheria yoyote inayowataka wenye mabasi kukataa kuwapakia wageni?
 
ufirauni wa akili na kukosa kujiamini kwa watendajiii !
Mabasi mengi sana hasa yanayotoka Ifakara hukamatwa na meno ya tembo ambayo abiria husafrisha ndani ya maboksi ya samaki, lakini hayafilisiwiii....Konda anajuaje huyu abiria si raiaa !?
 
Uonevu wa hali ya juu mabus yanayo safiri nchini huwa hawaulizi passport wala viza
 
Back
Top Bottom