Torra Siabba
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 243
- 287
Wana Jamvi kheri ya Sikukuu na mwaka mpya 2025. Kuna jambo naomba lilete kwenu hapa, juzi Desemba 24 nilikuwa miongoni mwa abiria zaidi ya 71 tuliosafiri na Basi la Nyehunge linalofanya safari zake Rulenge - Ngara - Mwanza.
Tulianza safari tu vizuri asubuhi lakini kumbe, mabasi haya yanayofanya safari zake eneo nililotaja, ni mabovu kiasi kwamba unajiuliza LATRA kwa kushirikiana na Trafiki wanaruhusuje haya magari kutoka stendi na kusafirisha Watu?
Tulipotoka eneo maarufu linalojulikana kama Munzani, Basi likazimika ghafla wakati likiwa kwenye mwendo, abiria wakapiga kelele weee, basi Mungu saidia likasimama, ndani ya Basi likaanza kutoka joto ambalo lilikuwa zaidi ya C38 jambo lililoongeza hofu kwa abiria ambao walitafuta pa kutokea.
Basi likasimama, wakaanza kulijaza maji kwenye rejeta nadhani (mimi sio mtaalaamu wa Mabasi) wamejaza zaidi ya dumu 25, basi linakunywa tu, baadaye chuma ikatengamaa tukaambiwa tupande tena.
Baada ya kupanda tulitembea kilometa zisizozidi tatu, tukasikia kishindo kumbe kuna Paipu ya Upepo ilipasuka, na hapo chuma ilikua mbio sana.. basi
CHUMA IKASIMAMA, HOFU IKATUJAA, Wachache waliokuwa na fedha za ziada wakatoa mizigo yao na kuamua kukodi usafiri mwingine nikiwemo mimi, sijui waliondoka pale sangapi..
Kwani kilichotokea ni kuwa Konda na Dereva kila Mtu alichukua usafiri wake na kuondoka alidai anaenda kutafuta 'spea'.
Kwahivyo ubovu wa haya magari ni mkubwa na kama Mamlaka hazitachukua hatua tutegemee siku za usoni ajali kutokea na kupoteza maisha ya watu.
Kwani taarifa ambazo tulikuja kuzipata baadaye ni kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kwa Abiria wa mabasi hayo kukutana na changamoto hiyo.
Alamsiki