DOKEZO Basi la Nyehunge linaloenda Ngara lisipoangaliwa litasababisha madhara ikiwemo kupoteza maisha ya Watu, LATRA fanyieni kazi hii hali

DOKEZO Basi la Nyehunge linaloenda Ngara lisipoangaliwa litasababisha madhara ikiwemo kupoteza maisha ya Watu, LATRA fanyieni kazi hii hali

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Torra Siabba

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2016
Posts
243
Reaction score
287
Wana Jamvi kheri ya Sikukuu na mwaka mpya 2025. Kuna jambo naomba lilete kwenu hapa, juzi Desemba 24 nilikuwa miongoni mwa abiria zaidi ya 71 tuliosafiri na Basi la Nyehunge linalofanya safari zake Rulenge - Ngara - Mwanza.

Tulianza safari tu vizuri asubuhi lakini kumbe, mabasi haya yanayofanya safari zake eneo nililotaja, ni mabovu kiasi kwamba unajiuliza LATRA kwa kushirikiana na Trafiki wanaruhusuje haya magari kutoka stendi na kusafirisha Watu?

Tulipotoka eneo maarufu linalojulikana kama Munzani, Basi likazimika ghafla wakati likiwa kwenye mwendo, abiria wakapiga kelele weee, basi Mungu saidia likasimama, ndani ya Basi likaanza kutoka joto ambalo lilikuwa zaidi ya C38 jambo lililoongeza hofu kwa abiria ambao walitafuta pa kutokea.

Basi likasimama, wakaanza kulijaza maji kwenye rejeta nadhani (mimi sio mtaalaamu wa Mabasi) wamejaza zaidi ya dumu 25, basi linakunywa tu, baadaye chuma ikatengamaa tukaambiwa tupande tena.

Baada ya kupanda tulitembea kilometa zisizozidi tatu, tukasikia kishindo kumbe kuna Paipu ya Upepo ilipasuka, na hapo chuma ilikua mbio sana.. basi

CHUMA IKASIMAMA, HOFU IKATUJAA, Wachache waliokuwa na fedha za ziada wakatoa mizigo yao na kuamua kukodi usafiri mwingine nikiwemo mimi, sijui waliondoka pale sangapi..

Kwani kilichotokea ni kuwa Konda na Dereva kila Mtu alichukua usafiri wake na kuondoka alidai anaenda kutafuta 'spea'.

Kwahivyo ubovu wa haya magari ni mkubwa na kama Mamlaka hazitachukua hatua tutegemee siku za usoni ajali kutokea na kupoteza maisha ya watu.

Kwani taarifa ambazo tulikuja kuzipata baadaye ni kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kwa Abiria wa mabasi hayo kukutana na changamoto hiyo.

Alamsiki
20241224_174904.jpg
20241224_174902.jpg
20241224_163108.jpg
20241224_163111.jpg
 
Wana Jamvi kheri ya skukuu na mwaka mpya ujao. Kuna jambo naomba lilete kwenu hapa.juzi desemba 24 nilikua miongoni mwa abiria zaidi ya 71 tuliosafiri na Basi la Nyehunge linalofanya safari zake Rulenge- Ngara- Mwanza.

Tulianza safari tu vizuri asubuhi lakini kumbe, mabasi haya yanayofanya safari zake eneo nililotaja, ni mabovu kupita kiasi na LATRA kwa kushirikiana na Trafiki wanaruhusuje haya magari kutoka stendi na kusafirisha Nafsi za watu?

Tulipotoka eneo maarufu linalojulikana kama Munzani , ile Basi ikazimika ghafla wakati ikiwa mwendo, abiria wakapiga kelele weee, basi Mungu saidia Basi likasimama, ndani ya Basi likaanza kutoka joto ambalo lilikuwa zaidi ya C38 jambo lililoongeza hofu kwa abiria ambao walitafuta pa kutokea.

Basi likasimama, wakaanza kulijaza maji kwenye rejeta nadhani (mimi.sio mtaalaamu wa Mabasi) wamejaza zaidi ya dumu 25, basi linakunywa tu, baadae chuma ikatengamaa tukaambiwa tupande tena. Baada ya kupanda tulitembea kilometa zisizo zidi tatu, Tukaskia kishindo kumbe kuna Paipu ya Upepo ikapasuka, na hapo chuma ilikua mbio sana.. basi

CHUMA IKASIMAMA, HOFU IKATUJAA TULIOKUWA WENGI, Wachache waliokuwa na fedha za ziada wakatoa mizigo yao na kuamua kukodi usafiri mwingine, sijui waliondoka pale sangapi...kwahivyo ubovu wa haya magari ni mkubwa na kama Mamlaka.hazitachukua hatua tutegemee siku za usoni ajali kutokea na kupoteza maisha ya watu. Alamsiki
PIGA SIMU TRAFFIC
 
Dah! Hiyo chombo inaonekana kweli imechoka aisee.
 
Sio huko tu mkuu, trend ya magari kuharibika njiani sasa hivi imekuwa kawaida nahisi kuna tatizo mahali mamlaka inapaswa ilitizame. Juzi kuna mahili nilikuwa natoka maeneo ya nyanda za juu kusini naelekea Mbeya gari ilizima maeneo fulani hivi safari ikaishia hapo maana wahusika walisema haliwezi kuendelea na hela washakusanya ilibidi wenye kujichanga tupande IT.
 
Ni umaskini tu ndio maana mnaletewe chuma mbovu...Nyehunge hazubutu kupeleka gari ya hivo Arusha,Moshi, au Mwanza Dar hakuna mtua atapanda tena hilo bus...nyie inaonekana mnapanda hamna option. Poleni.
 
Wana Jamvi kheri ya Sikukuu na mwaka mpya 2025. Kuna jambo naomba lilete kwenu hapa, juzi Desemba 24 nilikuwa miongoni mwa abiria zaidi ya 71 tuliosafiri na Basi la Nyehunge linalofanya safari zake Rulenge - Ngara - Mwanza.

Tulianza safari tu vizuri asubuhi lakini kumbe, mabasi haya yanayofanya safari zake eneo nililotaja, ni mabovu kiasi kwamba unajiuliza LATRA kwa kushirikiana na Trafiki wanaruhusuje haya magari kutoka stendi na kusafirisha Watu?

Tulipotoka eneo maarufu linalojulikana kama Munzani, Basi likazimika ghafla wakati likiwa kwenye mwendo, abiria wakapiga kelele weee, basi Mungu saidia likasimama, ndani ya Basi likaanza kutoka joto ambalo lilikuwa zaidi ya C38 jambo lililoongeza hofu kwa abiria ambao walitafuta pa kutokea.

Basi likasimama, wakaanza kulijaza maji kwenye rejeta nadhani (mimi sio mtaalaamu wa Mabasi) wamejaza zaidi ya dumu 25, basi linakunywa tu, baadaye chuma ikatengamaa tukaambiwa tupande tena.

Baada ya kupanda tulitembea kilometa zisizozidi tatu, tukasikia kishindo kumbe kuna Paipu ya Upepo ilipasuka, na hapo chuma ilikua mbio sana.. basi

CHUMA IKASIMAMA, HOFU IKATUJAA, Wachache waliokuwa na fedha za ziada wakatoa mizigo yao na kuamua kukodi usafiri mwingine nikiwemo mimi, sijui waliondoka pale sangapi..

Kwani kilichotokea ni kuwa Konda na Dereva kila Mtu alichukua usafiri wake na kuondoka alidai anaenda kutafuta 'spea'.

Kwahivyo ubovu wa haya magari ni mkubwa na kama Mamlaka hazitachukua hatua tutegemee siku za usoni ajali kutokea na kupoteza maisha ya watu.

Kwani taarifa ambazo tulikuja kuzipata baadaye ni kuwa hiyo siyo mara ya kwanza kwa Abiria wa mabasi hayo kukutana na changamoto hiyo.

Alamsiki
View attachment 3185572View attachment 3185574View attachment 3185576View attachment 3185577

Naunga mkono hoja mkuu, Route ya huko inaonekana na polisi wanakula Rushwa, mabasi yote ni mabovu hata zuberi,

Huwa wanapakia Abiria wengi sana wengine wanakaa mpaka katikati ambapo hakuna siti wengine wanasimama,

Wakifika eneo la Munzani wanashusha Abiria wote waliosimama wanaenda kupima gari baada ya kupima Abiria wanarudi tena safari inaendelea!
Ni kawaida yao magari kuharibika njiani, kuna siku tulisimama njiani karibu masaa manne gari mbovu hivyo hivyo pia tuliokua na vichenji ikabidi tipande hari zingine,

Hii nchi uozo mtupi ajari zinaanzia kwa matrafiki wemyewe
 
Back
Top Bottom