Basi la Simba SC lazuiwa,fans wamtaka wamuone Kichuya

Basi la Simba SC lazuiwa,fans wamtaka wamuone Kichuya

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
FB_IMG_1510149543558.jpg


Nyota ya Wnga wa kushoto wa Simba, Shiza Ramadhani Kichuya imeonekana kuendelea kuwaka kutokana na mashabiki wa timu hiyo mkoa wa Katavi kumuuliza licha ya yeye kutokuwa sehemu ya timu hiyo mkoani humo.
Mashabiki wa Simba ambao walijaa njiani wakati timu ikitoka Mbeya kwenda Katavi walikuwa wakilisimamisha basi la timu hiyo mara kwa mara huku wakimuuliza Kichuya alipo.

Kichuya ndiye aliyekuwa shujaa wa Simba mkoani Mbeya baada ya kuifungia bao muhimu kwenye mchezo wa ligi kuu mbele ya wenyeji wao, Mbeya City. Simba alishinda bao 1-0.

Kikosi cha Simba mkoani humo ambacho jana Jumanne kilicheza mechi ya kilafiki na timu ya Nyundo FC lilishuhudia umati mkubwa wa mashabiki wa timu hiyo mkoani humo wakiwa na hamu ya kumuona mshambuliaji huyo ambaye alikwenda kujiunga na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, kinachojiandaa na mechi dhiidi ya Benin.

Umati huo uliofulika kuipokea timu hiyo ulikuwa unamng’ang’ania kumuona Kichuya ambapo wengine walikuwa wanamuita jina lake sambamba na mshambuliaji mweza, Emmanuel Okwi raia wa Uganda ambaye naye hayupo baada ya kwenda Uganda.

Wachezaji ambao hawakuungana na Simba mkoani Katavi ni Aishi Manula, Jonas Mkude, Emmanuel Okwi, Juuko Murshid (wote wameenda Uganda) na Said Ndemla aliyeenda kwenye majaribio Sweden

Ikumbukwe kwamba Kichuya amekuwa ni kiboko ya Yanga SC baada ya kuwafunga mara tano mfululizo,mara zote akifunga magoli ya ajabu-ajabu yaliyopelekea mchezaji huyo kutungiwa wimbo
 
Wanaimba kichuya kiboko yaooo [emoji444] [emoji444] [emoji444] [emoji444]
 
Yule Mfanyabiashara aliyeuziwa timu kwa bei chee alkuwepo? cz naona amewafanyia usajili wa milion kadhaa akasema ni zaidi ya bilion wakasema ndiooo baada ya kula bscut na wali wa pale mkutanon ...
Cc. MANARA
 
Yule Mfanyabiashara aliyeuziwa timu kwa bei chee alkuwepo? cz naona amewafanyia usajili wa milion kadhaa akasema ni zaidi ya bilion wakasema ndiooo baada ya kula bscut na wali wa pale mkutanon ...
Cc. MANARA
Acha gubu pesa za kwako??
 
wakati basi la yanga linasimamishwa ili watu waonyeshwe Kombe la VPL....Huko kwenu wanataka kumuona Kichuya. hahahahaha TheDiferenceNoted.
 
Back
Top Bottom