Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Bus la wachezaji wa Dodoma Jiji FC limepata ajali likiwa njiani kutoka Mkoani Lindi kuelekea Jijini Dodoma, ajali imetokea katika eneo la kati ya Nangurukuru na Somanga wakati linatokea Ruangwa, Lindi walipocheza jana dhidi ya Namungo FC, kuna wachezaji wamejeruhiwa.
Akizungumza na JamiiForums, Msemaji wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema “Basi lilikuwa likitokea Luhangwa kuelekea Dar limepata ajali eneo la Matandu, limepinduka na kuingia mtoni katika Mti Matandu.
Watu kadhaa wamejeruhiwa, kati yao watatu ndio wana majeraha makubwa, wengine wote ni majeraha ya kawaida ikiwemo michuko na kukatwa na vioo.
Wale ambao hali zao ni mbaya wamechukuliwa na Ambulance wanapatikwa matibabu katika Kituo cha Afya cha Nangurukuru, ambao ni wachezaji wawili na viongozi.
===================================