Basi la Timu ya Dodoma Jiji lapata ajali kwa kutumbukia mtoni

Basi la Timu ya Dodoma Jiji lapata ajali kwa kutumbukia mtoni

Duuh hii ni ajabu sana jana tu wakati naangalia mechi yao na namungo niliwaza nikasema hivi hawa wachezaji wa hizi timu nyingine ukiacha simba na yanga, huwa wanapanda usafiri gani wakiwa wanaenda kucheza ugenini maana sidhani kama huwa wanakodi ndege na sijawahi kupishana na mabasi yao popote pale, akili ikaniambia pengine huwa wanapanda ndege kama abiria wa kawaida maana kusafiri na mabasi ni risk kumbe nilikuwa nawaza ambacho kinaenda kutokea leo..anyway nawatakia hao majeruhi wote uponyaji wa haraka!!
 
Madaraja ya Somanga, Masaninga, Nangurukuru yote yote yamezolewa na maji tangu mwaka jana na hayajajengwa. Yamejaza mawe tu kihuni...
 
So sad.
Ila kutokana na picha hiyo ubovu miundombinu inaweza kuwa chanzo cha ajali.
Ni kweli mkuu.
Hii sehemu ilipata athari ya mafuriko ya mwaka jana na bado hapajakaa vizuri.Kazi inaendelea niliona wiki iliyopita.
 
Halafu anatokea andazi mmoja anasema timu zisidhaminiwe na mdhamini mmoja hv hawa Dodoma kama wangekuwa na mdhamini wa maana c wangependa ndege
 
Kwani tunatumia Ndege ili tusipate ajali au kuokoa muda au uchovu?Hapa kilichotokea ni ajali suala la Ndege linahusika vipi?.Ajali inatokea tu tofauti ni ajali ya Ndege,ya Gari Boti n.k.
Halafu anatokea andazi mmoja anasema timu zisidhaminiwe na mdhamini mmoja hv hawa Dodoma kama wangekuwa na mdhamini wa maana c wangependa nd
 
Bus la wachezaji wa Dodoma Jiji FC limepata ajali likiwa njiani kutoka Mkoani Lindi kuelekea Jijini Dodoma, ajali imetokea katika eneo la kati ya Nangurukuru na Somanga wakati linatokea Ruangwa, Lindi walipocheza jana dhidi ya Namungo FC, kuna wachezaji wamejeruhiwa.
Ukanda huo si ndiyo ulimvukiza Mwendazake moshi akihutubia
 
Back
Top Bottom