Basil Mramba in graft probe

Basil Mramba in graft probe

Wote waliokuwa karibu na fisadi Mkapa wanahusika kwa namna moja au nyingine kwa ufisadi. Kuna mabalozi wawili mmoja aliteuliwa siku chache kabla ya fisadi Mkapa kumaliza muda wake. Mmoja yuko Sweden na mwingine US ambaye inasemekana alihamishiwa huko ili 'akasimamie biashara za fisadi Mkapa' US kwa ombi alilofanya fisadi kwa Muungwana. Pia inasemekana huyo ndiye aliyemuuguza alipokuwa kalazwa Switzerland. Hawa wawili nao ingekuwa vizuri nao wakachunguzwa maana sia ajabu wanajua mengi kuhusiana na ufisadi alioufanya fisadi Mkapa.

Bubu na wewe umeanza uoga kama kina this day?!!,,tunaomba majina ya hao jamaa wawili,, yaani wa sweden na huyo wa US,,,usiwe muoga hapa tunamkoma nyani giladi hata kama ni babamkwe...tafadhari mkulu
 
Yaani mabalozi wa Tanzania huko hawajulikani!?
 
Mie nashangaa hii serikali ya JK. Unamchunguza mtu kama Mramba wakati mwenzake Mgonja bado anakalia sofa pale hazina. Sasa huyo Mgonja hawezi kuharibu vielelezo ambavyo vinaweza kutumika kama ushahidi?? Maana Mgonja naye ni fisadi, na yote hayo yote ya EPA, Twin Tower na matakataka mengine yametokea under his watch. JK alitaadharishwa na JF pamoja na wananchi wengine juu ya Mzee wa VIJISENTI (CHENGE) lakini masikio yake yalikuwa na NTA. Matokeo yake yakawa ni aibu kwake. Sasa tusubiri ya MGONJA maana JK anajifanya kwa mara nyingine masikio yake kuwa na NTA.

Indume,

JK is a joke. Part of me is convinced that the reason he is taking so long to find a Chenge replacement is due to the fact that he wants to find somebody who can do a good cover up, but somebody who is not so obvious.
 
ATAKULA MAJANI GEREZANI, KAMA ASIPOENDA GEREZANI, TUTAWEKA Dynamite PALE KWAKE HILI TUMALIZE KAZI.
 
DPP okays move to prosecute Mramba: File back in PCCB's hands

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE office of the Director of Public Prosecutions (DPP) has given corruption investigators a formal go-ahead to file criminal charges against former finance minister Basil Mramba, it has been revealed.

Well-placed sources say the official consent to prosecute the veteran Rombo MP was issued to the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) some two months ago.

When contacted by THISDAY for comment earlier this week, the Director of Public Prosecutions, Eliezer Feleshi, confirmed that his office had already processed the application for permission to formally charge and prosecute Mramba, and forwarded the file to PCCB for action.

''I have already returned the file to PCCB?they are the competent authority to comment on this matter right now,'' said the DPP when asked to explain if he had given consent for prosecution.

He declined further comment on the subject.

However, government sources confirmed that the DPP's office had indeed given the formal consent paving the way for PCCB to prosecute the former minister on the basis of the evidence gathered in the course of its investigations.

Under the Prevention and Combating of Corruption Act of 2007, the PCCB can proceed with prosecution of suspects upon getting a written consent from the DPP's office.

The law requires the DPP to process an application for consent to prosecute from the PCCB within a maximum of 30 days.

The legislation also empowers the PCCB ''subject to the directions of the Director of Public Prosecutions [to] prosecute offences under this Act and other offences involving corruption''.

Efforts to get a comment from PCCB director general Dr Edward Hoseah on the anti-corruption watchdog body's next move proved futile yesterday.

Sources say the Mramba investigation has centred on his five-year tenure as finance minister in the third phase government of ex-president Benjamin Mkapa.

The 68-year-old senior politician held the key portfolio through the second and final term of the Mkapa administration, now hounded by allegations of controversial government contracts and dubious official payments worth hundreds billions of shillings, from the Treasury and the Bank of Tanzania.

It is understood that the investigations have already reached an advanced stage, with the PCCB now expected to make its next move.

Before being appointed finance minister, Mramba served as minister for industries and trade under Mkapa from 1995 to 2000.

From 2006, he served as minister for infrastructure development in the fourth phase government of President Jakaya Kikwete, later being reappointed minister in charge of industry, trade and marketing, before eventually being dropped after the dissolution and re-composition of the cabinet last February.

Some allegations that dogged the third phase government when Mramba was finance minister included the dubious contract with Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation; the external payment arrears (EPA) account scandal; and the 70bn/- military radar deal.

The Treasury was also at the heart of various other dubious deals including the BoT Twin Towers project, the purchase of the presidential jet, and controversial guarantees given by the central bank in favour of certain private companies.

Mramba in person has also been linked to the controversial 15-year extension of the Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) contract, known to have been personally ordered by Mkapa in late 2005.
 
JK is a joke. Part of me is convinced that the reason he is taking so long to find a Chenge replacement is due to the fact that he wants to find somebody who can do a good cover up, but somebody who is not so obvious.

Maskini Makongoro Mahanga,ameahirisha hata safari yake ya kwenda kutibiwa fungus za miguu akisubiri uwaziri
 
hahahaha nasikia mzee mzima BEN eti haifunction kabisaaa hana mambo kabisa ndo maana jamaa akawa anamchapia.
Eti ni kweli jamaa BEN ana mtoto kweli??kwani nasikia ndugu wa mamaa wanadai hana chake hata wa kusingiziwa sasa inabidi wapimwe DNA tujue tu jamani!!!

Are you serious?
 
Hii move ya kumprobe Mramba ni calculated to cleanse the govt baada ya wafadhili kutishia kuwithdraw msaada. PCCB waliichunguza RICHMOND, matokeo ilikuwa nini?
 
Huyu huyu alidiriki kutuambia ata nyasi mtakula Jet ya raisi lazima itue DSM.
Alikuwa kimya kitambo kumbe alikuwa na maana yake.
 
hata majani tutakula, lakini lazima Rada inunuliwe! Halafu anataka kujibaraguza

Mramba amlipua Mkapa!

2008-08-13 15:47:06
Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Katiaka kile ambacho pengine hakikutazamiwa kutokea, Waziri wa zamani katika Serikali ya Awamu ya Tatu ya Rais Benjamin Mkapa na ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rombo, Mheshimiwa Basil Mramba, amemlipua kiaina Rais Mstaafu Mkapa kwa kuiponda Serikali yake kuhusu sera ya viwanda.

Mheshimiwa Mramba amesema Serikali hiyo ya awamu ya tatu ( iliyokuwa ikiongozwa na Rais Mkapa), kamwe haikuwahi kutekeleza sera ya viwanda.

Akizungumza bungeni jana wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Mheshimiwa Mramba akazidi kueleza kuwa kwa kasi iliyokuwepo katika serikali ya awamu ya tatu, nchi ingechukua muda mrefu sana kuwa na viwanda.

``...Nina tatizo. Najua watu watauliza, si (nawe) ulikuwepo. Lakini wacha niseme,`` ndivyo alivyoanza kueleza Mheshimiwa Mramba kabla ya kuchangia zaidi.

Aidha, Mheshimiwa Mramba aliwageukia wajumbe wa Halmashauri ya CCM ,NEC na kuwahoji kuhusu sera ya viwanda vidogovidogo.

``Simuoni Bw. Yusuf Makamba, Katibu Mkuu wetu wa CCM... lakini nawaona wajumbe wengi wa Halmashaurii Kuu ya Taifa. Nauliza, hivi CCM ina Sera ya viwanda vidogo vidogo?`` Akahoji Mheshimiwa Mramba ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.

Akasema viwanda vilivyopo sasa ni matokeo ya sera za Serikali ya Awamu ya Kwanza iliyokuwa ikiongozwa na Rais wa wakati huo, Marehemu Mwalimu Nyerere.

Akasisitiza kuwa viwanda vingi vilivyopo leo ni vya Nyerere na kwamba sera yake ilikuwa ni viwanda vya awali, ambayo amesema kamwe haijatekelezwa katika serikali ya awamu ya tatu (ya Rais Mkapa).

Hata hivyo, Mheshimiwa Mramba akasema anafurahia kuona Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko ameipeleka bungeni, huku akishauri kuwa Serikali ya sasa ya awamu ya nne, ijielekeze katika jitihada za kuchochea uanzishaji wa viwanda.

Pia akaishauri serikali kusamehe kodi kwa viwanda vidogo vidogo kama inavyofanya kwa viwanda vikubwa ambavyo vimekuwa vikipata msamaha.

Aidha, ametaka kuanzishwa kwa benki maalum kwa ajili ya viwanda vidogo ama kuziagiza benki kutenga fungu maalum kwa ajili ya kuwakopesha wanaoanzisha viwanda hivyo.

SOURCE: Alasiri
 
Huku ni kutuzuga watanzania ili tumuone ni mtu safi, hivi kwa yote aliyoyafanya ambayo yamesababisha kwa kiasi kikubwa watanzania tukawa katika hali tuliyonayo, leo hii Mramba anadiriki hata kufungua kinywa chake na "kujiponda" yeye mwenyewe na wafuasi wake waliosababisha hali hii itokee? au anafikiria kwa kufanya hivyo ndipo ripoti ya EPA itampita pembeni na kutomtaja kama ni mshirika namba 2 or 3 wa sakata zima la EPA wakiongozwa na Mkapa na shangazi yao Zakhia Meghi?

kwa ufisadi waliofanya awamu ya tatu na ufisadi wanaouendeleza kwa kweli inatosha, wasubiri hadi tutakapofanikiwa kuwatoa hapo walipo, hatutaki kusikia ngonjera zao tena, tumechoka
 
Ni jambo gumu sana kumuamini Basil Mramba. Kama alivyosema yeye mwenyewe hiyo ilikuwa wizara yake, angesema alifanya nini kwanza alipoona hali hiyo akiwa serikalini kuliko kuongea ya Mkapa wakati ya EPA bado hajasema. He is trying to make a distraction.
 
Anayosema Mramba si mageni kwa wafuatiliaji wa kauli zake aliwambia wadanganyika kuwa hata majani wale lakini ndenge ya Rais lazima, pili aliataka kuiuza ATC kwenye kampuni ambayo yeye ni mmoja wa wamiliki alipomulikwa akakanusha alipotemwa kwenye uwaziri tukamuona akiwa Paris kwenye makabidhiano ya ndege ambayo kampuni yake ndiyo ilitaka kumiliki ikiwa na jina la jimbo lake " Rombo"achilia mbali akiwa waziri wa viwanda enzi za Nyerere alipigwa chini je inajulikana alichishwa kwa kwanini tufuatilie ujenzi wa viwanda vidogo vigodo Tanzania na ushiriki wa wake na kampuni moja ya ujenzi mkoani kilimanjaro, Lipi la kweli huyu ni fisadi tu Mr. $ 200,000/. Yetu macho wadanganyika tupo? Alamsiki
 
JAMANI MUNGU ADHIHAKIWI ATASIKU MOJA!!!!

Mramba ataka gazeti limlipe bil. 1/-

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Viwanda Biashara na Masoko Bw. Basil Mramba ameifikisha Kampuni ya Mwananchi Comunications Ltd. na baadhi ya watendaji wake Mahakama kuu akidai kuwa amechafuliwa jina na kudai kulipwa fidia ya sh. bilioni 1.

Hati ya mashitaka iliyoandaliwa na Wakili wa Bw. Mramba ambaye ni kampuni ya M. R. M. Lamwai ilidai kuwa habari zilizoandikwa na gazeti la Kampuni ya Mwananchi Comunications Ltd. la Sunday Citizen kumhusu yeye hazikuwa za kweli.

Tarifa hiyo ilisema, habari hiyo ilikuwa na kichwa cha habari kisemamcho "Mkurugenzi wa Kampuni ya Alex Stewarts ni Mtoto wa Mramba ?" na kichwa kingine kilichosema "Godfrey Mramba ni Mkurugenzi wa Alex Stewarts".

Ilisema gazeti hilo liliandika kwamba Meneja Mkuu wa kampuni ya Alex Stewart anayeitwa Godfrey Kaindoah ni mtoto wa Waziri Mramba na kwamba ametumia jina tofauti kuficha ukweli.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, gazeti hilo lilipoomba kuonana na Bw. Mramba kuhusiana na suala hilo, msaidizi wake alisema kwamba wamekubaliana habari hiyo isichapishwe.

Taarifa hiyo ilisema gazeti hilo lilidhamiria kuonesha kwamba Bw. Mramba akiwa Waziri wa Fedha, alishawishi Baraza la Mawaziri kukubali kuingia kwa Kampuni ya Alex Stewarts Assayers kwa ajili ya kukagua madini na hivyo hakustahili kuwa katika nafasi hiyo.

Taarifa hiyo ilisema Gazeti hilo lilitaka kuonesha kwamba Bw. Mramba alitumia vibaya nafasi yake ikiwemo kuchukua au kutoa rushwa kwa ajili ya kumpa mwanawe biashara.

Iliendelea kusema kwamba, gazeti hilo lilitaka kuonesha kwamba kampuni ya Alex Stewarts iliyopata mkataba wa kufanya kazi hiyo wenye thamani ya zaidi ya sh. bilioni 18 za Tanzania (Dola ya Marekani milioni 1, ilisababisha Serikali kupoteza kiasi kikubwa cha fedha za kigeni.

" Gazeti hili lilitaka kuonesha kwamba Bw. Mramba ni muhuni na ambaye amezaa mtoto nje ya ndoa na kuficha jina lake," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo ilisema, Bw. Mramba ameharibiwa jina lake kwa kuhusishwa na tuhuma ambazo ni sawa na kutenda kosa la jinai kwa kuhusika na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi.

Tarifa hiyo iliesema Bw. Mramba alitaka aombwe radhi na kulipwa lakini Kampuni hiyo ilikataa na kudharau mwito huo.

Mwanzoni mwa wiki hii, Bw. Mramba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari alisema kwamba atajiuzulu uwaziri kama ikithibitika kwamba Bw. Kaindoah ni mtoto wake.

Alisema kuwa hana mtoto anayeitwa Godfrey Kaindoah na kwamba yupo tayari kupima kipimo cha kutambua chembechembe za mwili zinazoonesha uhusiano cha DNA.
 
mbona hakwenda mahakamani kwa kweli alidhalilishwa?
 
Nadhani hata ukimuuliza sasa atakwambia bado ni waongo na atawashitaki. Hizo ndizo sura za kinyonga za mafisadi. Ngoma inogire!
 
Alichemsha hajui wenzake wanadai baada ya kwenda mahakamani na kushinda kesi,,sasa ajaenda anataka pesa,matokeo yake anadaiwa zaidi ya zile ambazo amedai....kazi kweli kweli,bongo akili!!!!
 
Back
Top Bottom