Basilla Mwanukuzi: Wakweli hawatakiwi nchini. Uongozi wangu ni kuweka maslahi ya wananchi mbele hata ikibidi kukosa cheo

Basilla Mwanukuzi: Wakweli hawatakiwi nchini. Uongozi wangu ni kuweka maslahi ya wananchi mbele hata ikibidi kukosa cheo

juma30

Senior Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
159
Reaction score
459
Na Basilla Mwanukuzi

KUNA CHA KUJIFUNZA

Aina yangu ya uongozi siku zote na muda wote ilijikita na itajikita katika kwanza kuweka mbele maslahi ya wananchi kwa gharama zote (hata ikibidi kukosa cheo)

2. Pili kuleta matokeo

Hakuna jambo kwangu ni hasara kama kua kwenye hali ya kutakiwa kuleta matokeo halafu kwenye mnyororo wa kuleta matokeo kuna watu wanaamua tu kua hayo matokeo sio shida zao...yani vile haraka ya nini??...hakuna matata...no hurry in Africa...ilihali wananchi wanaumia na kuteseka alafu na wewe ukaendelea kutulia tu kwenda na 'trend'

3. Kuleta matokeo kwa wakati
Muda ni kila kitu Serikali inafanya kazi kubwa MNO kuleta fedha kwa ajili ya wananchi inaleta fedha na muongozo mradi uishe ndani ya miezi 3. Inapaswa uishe ndani ya miezi 3 sana sana ukichelewa kidogo basi siku chache za nyongeza sio kama hapo ambapo ujenzi wa miezi 3 umechukua miaka 3 na fedha inaisha mradi haujaisha . Zahanati zote 3 . Wananchi wanateseka hawapati huduma
HAIKUBALIKI duniani wala mbinguni.

Uongozi ni dhamana, uongozi ni UTAKATIFU utakatifu uwe sio kwa mtu mmoja , ukiwa kwa mtu mmoja matokeo yake you will be THE ODD ONE OUT.
Uongozi ni UJASIRI

HASARA YA AINA HII YA UONGOZI (kama ni 'Hasara")
1. Utagombana na wote wenye maslahi yao hata ambao wanatakiwa kukuandikia taarifa zako (unaweza kuimagine watakachoamua kukuandikia ) kifupi utaharibiwa ma-file (uwe tayari)

FAIDA
Faida ni KUBWA ZAIDI utabaki na uadilifu wako na uaminifu wako , kwako , kwa nafasi yako, kwa mamlaka yako ya uteuzi, kwa WANANCHI, kwa Taifa lako, na kwa Mungu wako . Utakua na furaha na amani ya moyo

SWALI ambalo kila Mtanzania anatakiwa ajiulize kwa nini Mtandao wa wenye MASLAHI unanguvu ina maana kuna unakoanzia na kuna ukoishia. Ukideal na unakoishia unajikaanga na mbaya zaidi hata wanaotakiwa kuungana nguvu na wewe badala yake watakua wanaongeza mafuta ukaangike vizuri

Mwenyezi Mungu aendelee kumpa mwanga Mhe Rais wetu @samia_suluhu_hassan katika kuliongoza Taifa
Kumpa wasaidizi wenye mioyo safi kutoka kila NGAZI na kila IDARA na kuweka maslahi ya Taifa mbele. Ili tufike tunakotakiwa kufika kama Taifa

Instagra: basillamwanukuzi
 
Huyu ilikuwa lazima atolewe kafara niliona spidi yake ya kusimamia sheria na kusimamia uwajibikaji sasa huwezi jua labda hao wakurugenzi wake wanamkono mrefu juu kuliko yeye wakamchongea aondolewe yeye wao waendelee kuhujumu miradi ya wananchi
 
Mkuu wa Wilaya (Mstaafu?) hawezi kuandika Kiswahili fasaha!
Duh ulitaka aandikaje mkuu embu sahisha makoza yake tuone Ni yapi

Mnk unakuwa mjinga San

Mm huyu nimemuelewa Ni mbaya Kama hajasevj peza na Wala Hana miradi ya maana hapo lazm chuchu zake ziume

Ila Kama Ana apartment zake ddm au Arusha na mwanza bas Wala asiwaze kazi inendelee

Mm sitaki ujinga nnchi hi Ni magufuli ndio alikuwa kidgo aliwezeaa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom