Bastola ya Ray yazua hofu ukumbini

Bastola ya Ray yazua hofu ukumbini

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
KATIKA hali ya kushangaza, muigizaji Vincent Kigosi ‘Ray’ alizua hofu ya aina yake baada ya kutinga fulana fupi iliyosababisha silaha yake aina ya bastola kuonekana na kuwafanya watu waliomzunguka kujawa na hofu.Tukio hilo la aina yake lilitokea Jumamosi iliyopita katika ufukwe wa Escape One, Mikocheni jijini Dar kulipokuwa na uzinduzi wa video ya wimbo wa Nashindwa wa mwanamuziki Christian Bella ‘King of The Best Melodies’.

Mwanahabari wetu aliyekuwa akikusanya matukio ukumbini humo, aliwashuhudia watu waliomzunguka Ray wakionesha hofu yao pale fulana yake ilipopanda juu na kuiacha bastola yake aliyoichomeka kwenye suruali ikionekana bila kificho ambapo zaidi walihofia mazingira ya unywaji wa pombe uliokuwepo.

“Jamani hii si hatari na ‘masanga’ haya anayogonga hapa ukimkorofisha hata kidogo tu si anaweza kukushuti bila kuwaza nini kitatokea?,” alisikika mmoja wa watu waliokuwa wamekaa jirani na msanii huyo.Baadhi ya watu hao waliokuwa jirani na Ray aliyekuwa amekaa pamoja na msanii mweziye Jacob Steven ‘JB’, walionekana wakiondoka eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.

“Hapa si salama sana ndugu zangu bora tuondoke, unaweza hata ukamkanyaga bahati mbaya akakulipua makusudi,” alisikika jamaa mwingine aliyekuwa eneo hilo.Jitihada za mwanahabari wetu kuzungumza na Ray eneo hilo hazikuweza kuzaa matunda kufuatia mazingira ya unywaji pombe uliokuwepo, lakini alipotafutwa siku iliyofuata, simu yake iliita bila kupokelewa.
 

Attachments

  • 1429693009228.jpg
    1429693009228.jpg
    29.1 KB · Views: 1,063
Alibeba bastola alienda kuwinda au alikua anajilinda na Alshabab
 
Tanzania ina matatizo makubwa matatu, ukosefu wa ajira, ukimwi na vikaragosi vya bongo movie.
 
wananyang'anywa polisi bunduki za SMG sembuse yeye na kibastola chake!watu wengi wanamiliki silaha lakini matumizi yake hawayazingatii.

Haishauriwi kabisa kama unapistol mtu akujue,lakini siku hizi kaka zetu pistol wamefanya fasheni,atajitahidi kuinama inama ili mradi tu uione
 
wananyang'anywa polisi bunduki za SMG sembuse yeye na kibastola chake!watu wengi wanamiliki silaha lakini matumizi yake hawayazingatii.

Haishauriwi kabisa kama unapistol mtu akujue,lakini siku hizi kaka zetu pistol wamefanya fasheni,atajitahidi kuinama inama ili mradi tu uione
nilikuwa na shida sana ya mguu wa kuku sasa nishajua wapi nitaupata!
 
Ahahaa mkuu we mvizie tu Ray unaipata kirahisi kabisa@124 Ali
 
Mshamba tuu huyu,mwanamme mzima anajitia mkorogo...
 
Back
Top Bottom