Ushauri wangu mimi ni
1. Bata wanapototolewa usiwachie wazurule ili kupunguza risk za vitu kama magnjwa, kunguru, mwewe n wanyama wengine .subiri wakue kidogo uweze kuwaachia.
2. Banapotolewa wapatie antibiotics kwenye maji zile za kuanzishia vifaranga kama tetracolivit au neoxychick zitasaidia kupunguza infection zinazowakumba mara kwa mara.
3. Hakikisha usafi wa mabanda vyombo maji na chakula chao bata wako sensitive sana kwenye sumu kuvu (aflatoxicosis), magonjwa kama aspergilosis, botulisim, avian cholera yoote haya kuyaepuka yanaitaji usafi
4. Zaidi kuepuka magonjwa yatokanayo na vyakula watengenezee starter yako wapatie mpka wakishafika umri wa kuanzia mwezi mpaka miwili unaweza anza kuwapatia mavyakula mengine kama mabaki n.k.
5. Kuna magonjwa kama duck viral hepatitis na duck viral interitis haya yanashambulia sana mashamba na hua kuna chanzo zake lkn tz bado.
Naona wafugaji wa bata wanaenda kununua chanjo kwenye maduka ya mifugo wanapewa newcasttle ngumburo ndui n.k hapo hua mnapigwa bata awana hz case kbsa
Heshima yako Mkuu, hongera kwa mchango mzuri ambao umeutoa hapa, umeelezea vizuri Sana na naamini kwa mfugaji ambae atafata ushauri wako bila shaka ataona mafanikio ndani ya muda mfupi
ila ninapenda kuchangia katika hoja ya bata kutopata magonjwa ya Newcastle,Gumboro na Ndui, kuna sehemu nitaungana na wewe ila kuna sehemu nitapingana na wewe
Nianze kwa kuungana na wewe kuwa bata hawapati Gumboro, na ata wakipata inakuwa ni Gumboro serotype 2 ambayo sio pathogenic kwa bata hivo haitawadhuru
Tukirudi kwenye NDV na NDUI hapo nakupinga Mkuu, Bata pia wanaugua Newcastle pamoja na Ndui, ispokuwa utofauti unakuja kwenye strain ipi ambayo wameathirika nayo ili waoneshe dalili, kwa strain 1 na 2 ya Newcastle inaathiri Sana kuku kuliko bata, kwenye hizo strains bata wanakuaga na Natural immunity
hivo sikatai kwamba Bata wana sifa kubwa ya kuwa resistant dhidi ya Newcastle ila haina maana kwamba hawaugui au hawafi kutokana na Newcastle issue jnakuja ni Newcastle ipi? na kumbuka strains za hawa virus zinaendelea kuongezeka na Ndv 4 inaathiri Bata vizuri na hasa bata ambao ni vifaranga, na ubaya unakuja pale ambapo mfugaji anachanganya Bata na Kuku, maana Kama pandemic ya Newcastle itatokea it means Bata watakuwa carrier na Kuku ndio watakuwa wahanga wakubwa kutokana na uwezo wao mdogo wa kupambana na Newcastle ilihali bata wao wako vizuri, so bata atakuwa anafanya kazi ya kuambukiza tu Kuku
Kuhusu case ya Ndui kwa bata ata haiitaji kuifungulia mjadala kama ushafuga Bata au unakaa na jamii inayofuga bata, siku hizi imekuwa kawaida Ndui kwa bata, hiyo case inatokea Mara kwa Mara na wafugaji wanadeal nayo either pasipo kujua kuwa ni Ndui na wengine wanajua fika kuwa ni Ndui ila utofauti wake na Kuku ni kwenye Mortality na Morbidity
Ni sawa na case ya Corona tu, kuna strain ingine inaathiri sana America na ingine inaathiri sana Asia au Europe ila unakuta hizo zote athari zake zinakuwa ni ndogo endapo ataugua Mwafrika, so huwezi kusema mwafrika haugui Corona maana nawao wanakufa japokuwa kwa idadi ndogo compared na Europe na kwingine, hadi hapo natumai utakuwa umenielewa mkuu, na karibu kwa Hoja