Battery Low!!!!!

mayenga

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2009
Posts
4,118
Reaction score
1,970
Huyu ndo katoka kazini,kapokewa na mkewe kipenzi kambusu kampa pole ya kazi,mezani tayari kuna supu ambayo ni sharti mumewe anywe ili apunguze uchovu,mke huyu ini darasa la saba,ni juzi tu kajiunga na kikundi cha ujasiriamali.Pamoja na kutokujua lugha ya kigeni,uwezo wa kuitumia simu yake anao,hii pengine ni kwa sababu tu ya mazoea.

Mumewe kaenda bafuni kuoga baada ya kugonga supu,simu ya mumewe iko kitandani,mara ghafla inaanza kutoa mlio hafifu,kwakuwa mumewe yupo bafuni,mke huyu anaona ni busara kuangalia apigaye na ikiwezekana aipokee,ili baadae apate kumpa maagizo mumewe.Mke huyu anaposhika simu ya mumewe anaona inaita,lakini inaandika BATTERY LOW!!!!!!,kutokana na uhafifu wa mlio,mke anaamini kabisa kwamba simu inahitaji chaji,anachukua simu kwa mapenzi makubwa na kuiweka kwenye charge.Mwanaume anapotoka kuoga,anamshukuru mkewe mpendwa na kuzuga sana kuwa simu yake hiyo ya kichina haitunzi moto.

Siri ni kwamba,ni nyumba ndogo ya mwanaume,kwa jina la Doris(si jina halisi) ambaye ameseviwa kwa jina la Battery Low, alipiga kukumbushia pesa za nepi za mtoto(wa nje ya ndoa) alizoahidiwa,na mlio hafifu uliwekwa kwa makusudi mazima.

Kazi kwenu wanawake!
 
Dah umenichekesha sana asubuh hiiiii... Mayenga


Haya bwana!
 
Ama kweli huwezimchunga mwanadamu, ...........yaani kila kukicha ni mbinu mpya. Aksante mwayego mie pamoja na kujitia nimefika fom foo nisingeligundua hili duh..............Battery Low!! Waacheni wanaume waitwe wanaume katika hili kwa kweli.
 
Kama darasa alifuzu kapewa na cheti, lakini za mwizi ni 39.
 
Ha ha ha ha ha ha uwiiiiiiiiiiiii nimecheka mpaka basi dah hii mbinu nilikuwa siijui sante sana

LOL!....Dena Amsi ulishajiaminisha ume-note down mbinu zote nini? lol!!!!!

Ama kweli huwezimchunga mwanadamu, ...........yaani kila kukicha ni mbinu mpya. Aksante mwayego mie pamoja na kujitia nimefika fom foo nisingeligundua hili duh..............Battery Low!! Waacheni wanaume waitwe wanaume katika hili kwa kweli.

mnh, balaaa!!! kuna dalili kila mlio wa simu utasababisha alarm bells. ....lol!
Kina mama muwe na amani jamani, hiyo ni 2% tu ya wanaume wote.
 
LOL!....Dena Amsi ulishajiaminisha ume-note down mbinu zote nini? lol!!!!!

Nakwambia wewe acha tu nilijifunza humu kuna siku kulikuwa na thread ya mambo kama haya so nikadhani mbinu ndo hizo hiiya leo kiboko
 
Dah ama kweli hujafa hujaumbika.....watu wamekuwa wajasiliamali sana
 
haa haa nimecheka kweli, dah hii kiboko. kweli binadamu ni wabunifu ile mbaya, nisingeweza hata ku guess
 
Teh teh teh teh teh teh
 
Mshkaji umetuharibia dili kuanika kibuti ndani ya mtandao. sasa tunalazimika kutoka kivingine
 
Mbinu mpya kila siku, bora ihalalishwe kabisa ili msipate tabu za aina hiyo lol
 
mweee!
 
utandawazi wakina dada kuwen makini.........................
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…