mayenga
JF-Expert Member
- Sep 6, 2009
- 4,118
- 1,970
Huyu ndo katoka kazini,kapokewa na mkewe kipenzi kambusu kampa pole ya kazi,mezani tayari kuna supu ambayo ni sharti mumewe anywe ili apunguze uchovu,mke huyu ini darasa la saba,ni juzi tu kajiunga na kikundi cha ujasiriamali.Pamoja na kutokujua lugha ya kigeni,uwezo wa kuitumia simu yake anao,hii pengine ni kwa sababu tu ya mazoea.
Mumewe kaenda bafuni kuoga baada ya kugonga supu,simu ya mumewe iko kitandani,mara ghafla inaanza kutoa mlio hafifu,kwakuwa mumewe yupo bafuni,mke huyu anaona ni busara kuangalia apigaye na ikiwezekana aipokee,ili baadae apate kumpa maagizo mumewe.Mke huyu anaposhika simu ya mumewe anaona inaita,lakini inaandika BATTERY LOW!!!!!!,kutokana na uhafifu wa mlio,mke anaamini kabisa kwamba simu inahitaji chaji,anachukua simu kwa mapenzi makubwa na kuiweka kwenye charge.Mwanaume anapotoka kuoga,anamshukuru mkewe mpendwa na kuzuga sana kuwa simu yake hiyo ya kichina haitunzi moto.
Siri ni kwamba,ni nyumba ndogo ya mwanaume,kwa jina la Doris(si jina halisi) ambaye ameseviwa kwa jina la Battery Low, alipiga kukumbushia pesa za nepi za mtoto(wa nje ya ndoa) alizoahidiwa,na mlio hafifu uliwekwa kwa makusudi mazima.
Kazi kwenu wanawake!