Battery ya Router yangu inakaa masaa machache, nitumie power bank yenye 10000 Mah badala ya battery ?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Nina pocket router huwa naitumia katika shughuli zangu, uwezo wa battery yake umeshuka na sasa inakaa masaa mawili ama matatu tu.

Nina power bank ina 10000 Mah, nataka niwe naitumia badala ya battery ya hio pocket router.

kuna sehemu imeandikwa hivi
1682679315416.png

Je kitaalam ntakuwa nimetatua tatizo ?
 
View attachment 2602349

Je kitaalam ntakuwa nimetatua tatizo ?
Usb zinajua kuregulate voltage/Amps as long as router ina usb na powerbank ni usb hakuna neno.
 
Unavyo zidi kuongeza mAH maana yake unaongeza muda wa matumizi.

Kikubwa zingatia kama Output Voltage za hiyo power bank unayotaka kutumia sasa zinaendana na kifaa chako.

Kama voltage ipo sawa basi utakua umetatua tatizo sababu the higher the mAH of a battery the more the time you get.

Karibu.
 
Power bank imeandikwa hivi mkuu, napata wasi wasi maana kwenye router imeandikwa 5V-1A.

Type-C Input : 5V-3A / 9V-2A
Type-C Output : 5V-3A / 9V-2.22A / 12V-1.5A
USB Output : 4.5V-5A / 5V-4.5A / 9V-2A / 12V-1.5A
Total Output : 20W
 
Usb zinajua kuregulate voltage/Amps as long as router ina usb na powerbank ni usb hakuna neno.
Power bank imeandikwa hivi mkuu, napata wasi wasi maana kwenye router imeandikwa 5V-1A.

Type-C Input : 5V-3A / 9V-2A
Type-C Output : 5V-3A / 9V-2.22A / 12V-1.5A
USB Output : 4.5V-5A / 5V-4.5A / 9V-2A / 12V-1.5A
Total Output : 20W
 
Power bank imeandikwa hivi mkuu, napata wasi wasi maana kwenye router imeandikwa 5V-1A.

Type-C Input : 5V-3A / 9V-2A
Type-C Output : 5V-3A / 9V-2.22A / 12V-1.5A
USB Output : 4.5V-5A / 5V-4.5A / 9V-2A / 12V-1.5A
Total Output : 20W
Haina neno as long as ni Usb kwa usb
 
Power bank imeandikwa hivi mkuu, napata wasi wasi maana kwenye router imeandikwa 5V-1A.

Type-C Input : 5V-3A / 9V-2A
Type-C Output : 5V-3A / 9V-2.22A / 12V-1.5A
USB Output : 4.5V-5A / 5V-4.5A / 9V-2A / 12V-1.5A
Total Output : 20W
Tumia USB port output yenye 5V-4.5A
 
Kuhusu router kundikwa 5V-1A, maana yake inahitaji supply au chanzo cha umeme chenye Volt 5 na kisiwe chini ya Ampere 1

Hivyo kwa hiyo Bank yako inafaa kama tuutatumia USB output port yenye 5V na Ampere Kuanzia 1 na kuendelea
 
Ina tundu moja tu ila hilo tundu ndio limeandikiwa linatoa hizo output zote, sasa sijui powerbank itajuaje
 
sasa sijui powerbank itajuaje
power bank ina PD-IC, by default itatoa 5V ( kwa 4.5 amps )
kama hiyo router yako ingekua na hii PD-IC ingemwambia powerBank, sitaki 5V , nataka 9V ( kama router ingekua rated 9V )
powerBank ingetoa 9V ( at 2 amps )

kwakua router haina PD-IC kwenye mfumo wake wa USB
powerbank itatoa default voltage ie: 5V ( at 4.5 amps )
kwa hivyo 5V ( 4.5 amps ) itamudu vizuri mzigo wa 5V ( 1 amp )
 
Back
Top Bottom