ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
Mwisho unatakiwa uelewe
Nioneshe jinsi Magufuli aliwawezesha Wachimbaji wadogo Kwa pesa na mitambo Ili na Mimi nikuoneshe alichofanya Samia maana rekodi zipo.
Unazunguka zunguka kuhusu Magufuli kujenga shule au Vyuo, ukweli ni kwamba hakuna Chuo kilichojengwa awamu yake na hata sekta ya Afya haikuoewa uzito kama ilivyo awamu ya 6 Kwa kujenga Hospital za Wilaya Kila Halmashauri,Vituo vya Afya zaidi ya 400 ,Maelfu ya Watumishi na Vifaa tiba vya Kisasa.
Miaka 6 ya Magu hii hapa 👇👇
Mwisho hakuna namna utaweza mlinganisha Samia na Magu kwenye delivery,kichaka chenu Kwa Sasa ni blaa blaa za Watumishi na sijui Shilingi imeshuka.
Ila sekta zifuatazo Samia Yuko level zake
-Elimu
-Afya
-Uchumi,Biashara & uwekezaji
-Barabara hasa Vijijini (TARURA)
-Kilimo na Uvuvi
-Maji
-Umeme na Nishati Safi ya Kupikia.
-Mapato
-Utalii
-Sekta ya Anga
-Ajira
Wewe una matatizo na shida kubwa ya uelewa.Nikikuuliza swali dogo tuu hapa hutonipa majibu.Hilo la elimu lote mimi nalifidia kwa sera ya Magufuli ya elimu bure.
Utambue kuwa unapoweka huduma fulani bure serikalini kunatakiwa kuwe na fungu la uendeshaji hiyo huduma.
Kuna vituo vya afya hususan maeneo ya vijijini vingi tu vilijengwa kipindi cha Magufuli na hata mimi nimeshuhudia.
Morogoro mkoa naotembea sana kuna vituo vya afya vitatu vilijengwa kwa wakati mmoja katika vijiji vitatu vinavyofuatana mnamo 2017 kama sijakosea.
Pia kuna vifaa tiba muhimu kama CT-Scan nahisi vilianza kuingizwa ama kuagizwa kwa wingi kipindi cha Magufuli.
Sera ya kubobeza madaktari ili wabaki katika vituo vyao badala ya kuandika rufaa lukuki kwa wagonjwa hili lilianza kipindi cha Marehemu Magufuli.
Hapa sasa ndio patamu zaidi mkuu.
Hivi umeshajiuliza pesa za kulipa hao watumishi wa umma na kuajiri zaidi zinatoka wapi!?
Mnafurahia mishahara mikubwa pasi na kujua wapi inatoka.
Kwa pato gani la taifa kila awamu uongeze mishahara!?
Mwishowe mnakopa na nchi inazidi kuwa na madeni baadae kupelekea devaluation ya shilingi yako.
Magufuli alishasema wazi,serikali ya Tanzania haina hizo pesa kiuhalisia za kuongeza mishahara kila wakati na kuajiri kila wakati.
Ila usisahau kuwa aliwapa kipaumbele wajasiriamali wadogo wadogo na vijana na kina mama kwa kuwapa fedha za mikopo kutoka Halmashauri.Hili jambo halikuanzia kwa Samia lilianzia kwa Magufuli.
Alitengeneza mazingira wezeshi ya hadi wa mtu wa chini kupata pesa.
Ila uliza sasa hivi hali ikoje mtaani.
Mimi kila leo naingia ofisi za utumishi wa umma.
Sijaona huo uhaba unaousemea zaidi ya kurudi kwa uzembe na kutokujituma kwa watumishi wa umma na kukosa nidhamu ya utumishi wa umma.
Usiseme miradi midogo unakosea hilo.
*Ufufuaji wa reli ya Kaskazini Arusha.
-Uboreshaji wa reli kuwa continuos welded kutoka kuwa jointed rail.
Maana hii reli Kikwete aliirudisha toka kwa wahindi ikiwa mufrisi.
*Uboreshaji wa bandari.
*Uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati.
*Uboreshaji wa sekta ya madini kwa kuweka mashine ya usafishaji dhahabu kuwa 99.99% pure na uozeshaji wa makinikia.
-Kuwapa fursa wachimbaji wadogo wadogo wa kufanya biashara ya madini na kupata mikopo wezeshi ya kuwezesha shughuli zao.
Hii unasema ni miradi midogo mkuu!??
Aya endeleeni kufurahia serikali za danganya toto kukopa ili iwaongezee mishahara na ajira ilhali nchi inaoza.
Nioneshe jinsi Magufuli aliwawezesha Wachimbaji wadogo Kwa pesa na mitambo Ili na Mimi nikuoneshe alichofanya Samia maana rekodi zipo.
Unazunguka zunguka kuhusu Magufuli kujenga shule au Vyuo, ukweli ni kwamba hakuna Chuo kilichojengwa awamu yake na hata sekta ya Afya haikuoewa uzito kama ilivyo awamu ya 6 Kwa kujenga Hospital za Wilaya Kila Halmashauri,Vituo vya Afya zaidi ya 400 ,Maelfu ya Watumishi na Vifaa tiba vya Kisasa.
Miaka 6 ya Magu hii hapa 👇👇
Mwisho hakuna namna utaweza mlinganisha Samia na Magu kwenye delivery,kichaka chenu Kwa Sasa ni blaa blaa za Watumishi na sijui Shilingi imeshuka.
Ila sekta zifuatazo Samia Yuko level zake
-Elimu
-Afya
-Uchumi,Biashara & uwekezaji
-Barabara hasa Vijijini (TARURA)
-Kilimo na Uvuvi
-Maji
-Umeme na Nishati Safi ya Kupikia.
-Mapato
-Utalii
-Sekta ya Anga
-Ajira