Unaweza kueleza ilikuwaje kipindi cha Magu hakukuwa na wizi?
Kuhusu hii ya kikwete kwenye barabara, iko technical kidogo. Kumbuka waziri aliyesimamia hizo barabara alikuwa huyo huyo Magu. Kwa haki ya marais wote wawili tungelinganisha miradi mingine ya kikwete ambayo haikuwa chini ya wizara ya ujenzi.
Kaka, hatukatai anayoyafanya mama Samia, kuendeleza ya miradi ya awamu ya tano, ambaye yeye mwenyewe alihusika. Tofauti ya Magu na wengine ni kuwa miradi yake ilikuwa ni a game changer, yaani alifanya paradigm shift kwa watanzania na Afrika kwa ujumla, kuwa tunaweza. Yale mambo ya kuwa Afrika mashariki haki yetu ni treni za garimoshi alituopa kule.
Ndiyo maana hadi watu wa mataifa wakaja na slogan za "magufulieffect" na "what would magufuli do". Nitajie kiongozi mwingine wa Africa aliyepewa hash tags kama hizo?