President of China
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 34,781
- 94,550
Kaka hakuna mtu yeyote humu aliyekwambia usimpinge Rais kulingana na uelewa wako. But between line ya maelezo yako yamejaa chuki nzito ambayo haijawahi tokea tangu ulimwengu uumbwe.Toa ushahidi ni mwanamke yupi nimemuonesha dharau?
Unatoa tu shutma bila ushahidi.
Hapa tunaongelea kiongozi wa taifa, where future yetu na watoto wetu iko mikononi mwake. Sasa kumpinga sio dhambi na yeye sio rais wa kwanza kupingwa or kukosolewa. Ni rais yupi hajawahi kukosolewa Tanzania?
Kuleta hoja ya yeye ni mwanamke ni shortsightedness.
Je, ni kipi kinachokufanya useme Rais Samia IQ yake ni ndogo? Huna sababu yoyote kaka. Ili kukuona huna sababu yoyote ni pale unapokuza trivial issue ya yeye kuacha kulieleza kwa kina swali la mwandishi wa habari alipomuuliza kuhusu sanction.
Wakati Rais ilizungumza mengi sana huko Urusi. Alitoa hotuba kwenye jukwaa kubwa St. Petersburg International Economic Forum (SPIEF). Jukwaa hilo lilihudhuriwa na watu zaidi ya 20,000.
Vilevile alihutubia chuoni.
Wewe umeng'ang'a na swali la sanction tu.
"Unasema mambo ya kudharau wanawake hujayasema." Kaka dharau haisemwi dharau inaonekana na sisi tunatafsiri, kinachotakiwa ujitanbue na urekebishe tabia hiyo mbaya.
Badilika kaka utaanza kuona dunia kwenye picha nyingine tofauti.
Na ninakusihi hebu tujadili kwa kina hii visit ya Rais huko Urusi kama kweli wewe ni mzalendo kuliko trivial issues.
Asante