- Tunachokijua
- BAVICHA ni baraza la vijana la Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baraza hilo lilifanya uchaguzi wa viongozi terehe 14 Januari, 2025 na kumchagua wakili Deogratius Mahinyila kuwa mwenyekiti wa Baraza hilo kwa ngazi ya Taifa.
Kumekuwapo na barua ambayo mdau amehitaji kujua halisia wake ikidaiwa kuwa imetoka kwa BAVICHA yenye lengo la kutoa dira na muelekeo wa baraza hilo chini ya uongozi wa mwenyekiti mpya Taifa Wakili Deogratius Mahinyila.
Uhalisia wa barua hiyo ya Bavicha upoje?
Baada ya kufuatilia barua hiyo iliyowasilishwa na mdau, JamiiCheck imebaini kuwa taarifa na barua hiyo si ya kweli. Kupitia ufuatiliaji wa kimtandao tumebaini kuwa barua hiyo haijachapishwa katika chanzo chochote cha kuaminika ikiwemo mitandao ya kijamii ya Bavicha.
Aidha JamiiCheck imewasiliana na Apollo Boniface ambaye ndiye anayeonekana kuwa ameandika barua hiyo kwa niaba ya Chadema katika nafasi ya afisa habari wa Bavicha. Apollo amesema;
Hiyo barua sio ya kwangu, imetengenezwa na watu kwa madhumuni wanayoyajua wao, pia mimi sipo kwenye hicho cheo kwa sasa.