Cvez
JF-Expert Member
- May 19, 2018
- 4,405
- 13,411
Katika moja ya mistake kubwa ilifanyika ni kuanza harakati za Katiba Mpya wakati wanachama wameparaganyika. Enzi za Mwendazake ilikua kufanya siasa ni dhambi kiasi ambacho wengi ya wapinzani waliamua kukaa kimya na kuendelea na maisha yao ya kila siku kwa usalama wao na familia zao. Walioendelea na siasa za upinzani ni wale pekee ambao siasa ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Mungu si Athumani Mwendazake akaenda mwangaza ukaonekana kidogo ingawa kiuhalisia utawala bado ni ule ule japo huu una nafuu, na hapa CDM ndipo walipokosea badala ya kuwarejesha wale wanachama waliopotezea siasa. Wakajiingiza kwenye Katiba Mpya si kitu kibaya ila kuna hatua zilitakiwa zifuatwe kama kuzunguka mashinani na kufanya mikutano ya ndani ili kurejesha ari ya wanachama wao.
Ni kweli walianza kidogo na mikutano ya ndani kanda ziwa, ila ghafla wakabadilisha gia angani na kuingia na Katiba Mpya na hapa ndio waliharibu, najua CDM wengi watapinga.
Baada ya brain ya movement yote kupigwa pini sasa hivi ni kurukia kila ajenda ndani ya siku 7 hizi, walikua na ajenda ya ZZK, ikaja kukosoa Royal Tour, jana mchungaji Mwigira kawapa mjadala pia. Kesho huenda Rais akapiga selfie na wajukuu zake najua wataruka nayo pia. Kiujumla kila kitu shaghala baghala wanaishi kwa trends. Kwa mwendo huu CCM watawapa topic kila wiki ya kujadili na kuacha kufanya mambo ya msingi.