msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 862
- 1,264
Na Wakili Charles N. Heche
Mwaka 2023, aliyekuwa Mwenyekiti wa BAVICHA, John Pambalu, alitua katika Uwanja wa OR Tambo kuhudhuria semina akiwa na timu ya rafiki zake. Ni katika kipindi hicho Operesheni ya CHADEMA ilisimama kwa sababu chama kilikosa fedha za usafiri na posho kwa wajumbe. Swali kubwa kwa vijana likawa, kwa nini fedha za operesheni ya kujenga chama zinakosekana, ilhali fedha za Pambalu kula bata South Afrika zinakuwepo? Huu ni usaliti mkubwa.
Wakati akiwa na umri wa miaka 34, Marehemu Edwini Mtei alikuwa Gavana wa Benki Kuu na baadaye akaasisi CHADEMA. Leo, kiongozi wa vijana wa CHADEMA mwenye umri wa zaidi ya miaka 34 (Twaha Mwaipaya) yuko mtandaoni akijihusisha na online pornography/masturbation. Vijana wa CHADEMA wamenajisi sababu za kuanzishwa kwa CHADEMA, hawafai hata kuruhusiwa kushiriki ibada ya msiba.
Katika uchaguzi wa ndani ya CHADEMA mwezi Januari 2025, wagombea wote vijana walipaswa kueleza upande waliopo ili kuungwa mkono katika uchaguzi.
Ulipaswa kueleza kama wewe ni wa Freeman au wa Lissu, si kupimwa kwa hoja na uwezo kama ilivyokuwa shabaha ya kuanzishwa kwa CHADEMA. Sote tumeona matokeo ya mfumo huo wa kipuuzi, ambapo BAVICHA waliishia kupata Mwenyekiti kutoka kundi la Lissu, Deo Mahinyila, ambaye mpaka sasa anashikilia rekodi ya kuwa kiongozi mbovu zaidi kuwahi kutokea.
Vijana wa CHADEMA siyo tena “think tank” ya chama; ni bendera fuata upepo. Wamesaliti dhamira halisi ya kuanzishwa kwa CHADEMA, ndiyo maana sioni kama wanatakiwa waruhusiwe hata kukanyaga nyumbani kwa Marehemu Mtei. Mwisho, si kwa umuhimu, Mtei ni mkwe wa Freeman Mbowe ambaye, licha ya kujitoa kwa chama chake kwa zaidi ya miaka 20, vijana hawa wa hovyo wamekuwa wakimtukana usiku na mchana. Wasaliti.
NB: Vijana karibu 17 wako Nairobi wakilipwa na Maria Sarungi kwaajili ya kutukana na kubagaza nchi yetu bila haya. Usaliti mkubwa kwa Chadema na Taifa kwa ujumla.