Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mambo yanazidi kunoga wakati tunaelekea 2025.
===
Siku moja tangu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tanzania Bara Tundu Lissu atangaze nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa katika mchakato wa ndani wa uchaguzi unaoendelea leo, Ijumaa Desemba 13. 2024 Baraza la Wanawake la chama hicho (BAWACHA) mkoa wa Mbeya limesema linamuunga mkono kwenye dhamira yake hiyo kwa kuwa anatekeleza haki yake ya Kikatiba.
Akizungumza na wanahabari mkoani humo, Mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Mbeya Elizabeth Mwakimomo amesema yeye kama mwanachama na kama kiongozi anatambua kuwa hiyo ni haki yake ya msingi.
"Sio jambo baya yeye (Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara na mtia nia wa nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Taifa) kugombea nafasi ya Mwenyekiti lakini ni utaratibu tu, ni utaratibu ambao unatakiwa kusubiriwa pindi uchaguzi utakapotangazwa watu watagombea kwa sababu chama chetu kina demokrasia" -Mwakimomo
Pia soma: Tundu Lissu atangaza nia ya kugombea nafasi ya uenyekiti CHADEMA
Akizungumzia suala la ukomo wa madaraka ambalo ni sehemu ya ajenda za Lissu, Mwenyekiti huyo wa BAWACHA mkoa wa Mbeya amesema suala hilo ni la Kikatiba, na kwamba Katiba ya chama hicho haijaweka ukomo wa madaraka badala yake imeacha wazi kwa kusema kuwa kila mtu anayo uhuru wa kugombea
"Kwenye hili suala la ukomo wa madaraka labda tuende kwenye mabadiliko ya Katiba yetu kwamba tuende tukabadilishe hicho kipengele ili kuwe na ukomo wa madaraka kama ni miaka miwili iwe miwili, kama miaka mitano iwe mitano, kwa hiyo suala la ukomo wa madaraka pia ni jambo jema" -Mwakimomo
Aidha, Elizabeth Mwakimomo amesema mtazamo wake anaona wazi kuwa Tundu Lissu yuko sahihi, kwa kuwa ni wengi wanataka kuona nafasi za Viti maalum vinakuwa na ukomo (Wabunge na Madiwani wa Viti maalum) ili watu wengine waweze kupata nafasi kwa sababu mara zote wamekuwa wakisema kila mmoja apate nafasi ya kupata nafasi ndani ya chama hicho
"Kwa hiyo inaweza kuwa miaka mitano, au miaka miwili basi, tuwe na ukomo isiwe miaka 10, miaka 20 kama mimi basi niwe mimi tu hapana, wakati kuna mtu mwingine pia hiyo nafasi anatakiwa akomazwe katika huo utaratibu" -Mwakimomo