Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Hawa watu kama wanafikiri kuteka na kuua watu ndio kutafanya watu wawe waoga, kwa hakika wanakosea sana, na aliewashauri aliwadanganya kwa kutokuja na kwa kutofanya research ndogo tu kujua kama vitendo hivi sehemu zingine duniani zimewahi kuwa msaada kwa watawala.
Hapa napoandika, huko Tanga, kina mama wa CHADEMA(BAWACHA) walikusanyika na kuanza kuimba, " hakuna muaji kama SSH (wakimtaja kwa jina) na hatakuwepo" .
Kwa kifupi, hawa wamama wakiwa kundi, wameimba hivyo mchana kweupe bila hofu wala woga(clip iko katika akaunti ya Ntobi wa CHADEMA kwenye mtandao wa X) na imepostiwa siku ya jana.
Ukiacha hawa wamama, utagundua tangu mauji ya mzee Kibao yatokee, watu mitandaoni wameendelea kufunguka na ukosoaji ndio umeongezeka tena kwa lugha kali zaidi na kwamba watu wanaona hawana tena cha kupoteza.
Siku zote iko hivi: unapoua au kutesa watu kwenyemaandamano, n.k, wanaobaki hugeuka kuwa ndugu moja na hivyo inakuwa rahisi kuungana huku wakiamini hawana tena cha kupoteza. Kwahiyo, hata wale waliokuwa na hofu, nao huoni ni bora kama ni kufa nao wafe tu kwani kama ndugu na jamaa zao(majirani, n.k) teyari wamekufa, kuna shida gani na wao wakifa?
Hii spirit ndio ambayo huchochea maandamano duniani kote Kwasbabu risasi na mabomu yanayotumika kumwaga damu, ndio hegeuka nguvu ya kuwaunganisha watu badala ya kuwarudisha nyuma.
Hivyo, kuteka na kuua, sio strategy sahihi ya kuwanyamazisha watu ili muwatawale, bali ni miscalculation ya hesabu zenu za kubaki madarakani, na kama ni mtihani, basi mmeshafeli vibaya.
BAWACHA mkoani Tanga wameonysha mfano, sasa endeleni.