Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu salaam,
Hivi mlifikiria nini kumualika Rais Samia kama mgeni rasmi na mpaka mkampa tuzo? Mlishauriana kwwli mkaona hii ni good move na italeta matokeo chanya mbeleni? Yaani mnafikiria kama sio wanasiasa, hamna stratergy kabisa, ni kama watu mnaofanya vitu utafikiri hamna vichwa.
Mambo ni haki yenu yaliyopokwa kinyume na sheria, mkashangilia na kumtukuza mpaka mkawa hamna tofauti na akina Lucas Mwashambwa kushangilia mpaka mnabubujikwa na machozi (halafu wananchi wakiwaita CCM B mnakasirika)!
Sasa mmekosea kule, mkazinduka mmekuja kufanya madudu mengine tena🤦♂️! Kuna watu wanahali ngumu sana nchini, vitenge mlivyochoma vingeenda saidia wanawake wangapi? Mmeona Rais Samia kawaangusha mngechomoa tu sura yake pale parts zingine zikafanyiwa namna, walau hata wananchi wangeona hata kama mmeharibu bado mnafikiria kwa maslahi yao. Mgetafuta namna ya kufikisha ujumbe wenu huku maslahi ya umma yakiwa lengo namba 1.
Ni sawa na wale mtu analima kwenye kiwanja cha mtu mwingine mazao yamenawiri wanaenda kufyeka na kuyaharibu, wakati yangeweza kutumika kwa namna nyingine huku pia aliyefanya kosa anatumikia adhabu yake.
Yaani nyie CHADEMA kwa ujumla mbali na kulalamika kila kukicha na kurushiana vijembe na CCM hamna kitu mna offer kwa wananchi kutatua changamoto zao. Walau ACT Wazalendo huwa wanakuja na solution kwa changamoto wanazozitoa, lakini CHADEMA na wengine ni bure kabisa.
Leteni hayo mapovu kwa breki😅!