PreGE2025 BAWACHA mwingine asemekana kushambuliwa na kikundi kilichopo chini ya Mwenyekiti wa CHADEMA Ilala

PreGE2025 BAWACHA mwingine asemekana kushambuliwa na kikundi kilichopo chini ya Mwenyekiti wa CHADEMA Ilala

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Wakuu,

Mbona kama kuna ka upepo kanatengenezwa hivi!🤨🧐🤔


Kamanda Lilian Byebalilo (BAWACHA) ameshambuliwa kwa kupigwa na watu wa Taskforce iliyopo chini ya Waziri Mweneviale (Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Ilala), shambulio hilo limepelekea Lilian kupoteza fahamu na kukimbizwa hospital kwa ajili ya matibabu kwa muda wa takribani masaa tano katika Hospitali ya JEMSA iliyopo Segerea.

Pia, Soma: Ghasia Ndani ya CHADEMA: Mwenezi wa BAWACHA Taifa ashambuliwa na Walinzi wa Heche

Na kisha kupewa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Amana iliyopo Ilala kwa ajili ya hatua zaidi za matibabu na uchunguzi wa afya yake hii ni mara ya pili kwa tukio la namna hii kutokea baada ya tukio lile la kwanza la kushambuliwa kwa mwenezi wa BAWACHA Taifa Siglada Mligo.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Polisi soon mnakwenda kujiunga kufanikisha sinema hizi za mwaka 1957 sreaaring Rashid Kawawa.
 
Huijui CCM wewe na kitu inachoweza kufanya ili kubaki madarakani, refer ile case ya sabaya kutafuta watu na kuwavalisha jezi za Chadema akawatuma kuharibu shamba la mbowe ili ionekane ni vijana wa Chadema, wanauwezo wa kufanya vitu vikubwa na vibaya zaidi
Chadema bhana 😂
Kila kitu mnasingizia ccm, kwa hao watu ni wapya hapo Chadema?
N lini mtapata akili timamu nyie?
 
Huijui CCM wewe na kitu inachoweza kufanya ili kubaki madarakani, refer ile case ya sabaya kutafuta watu na kuwavalisha jezi za Chadema akawatuma kuharibu shamba la mbowe ili ionekane ni vijana wa Chadema, wanauwezo wa kufanya vitu vikubwa na vibaya zaidi
Nasikia pia ccm ndo walimtoa mbowe uenyekitini 😎
 
Kamanda Allen Kilewella, fanya uwasiliane na Makamanda wenzako wa chama akiwemo Mwenyekiti Mpya Kamanda Tundu Lissu, ili mfikie muafaka na hawa Bawacha, pamoja na makundi mengine yaliyokuwa nyuma ya Mwenyekiti aliyeondoka madarakani (Mh. Mbowe).

Ninachokumbuka wakati wa kampeni, hawa Bawacha wa sasa walikuwa upande wa Mbowe! Msipochukua hatua mapema ya kufanya maridhiano, mtakuwa mnaenda mbele na kurudi nyuma kutokana na hujuma mtakazofanyiwa na haya makundi yanayo endelea kuwapinga hata baada ya uchaguzi kumalizika.
Uko sahihi kabisa. Kwa kweli haileti picha nzuri.

Amandla...
 
Back
Top Bottom