BAWACHA wamchongea kwa Rais mkurugenzi aliyewatimua wasipande miti

BAWACHA wamchongea kwa Rais mkurugenzi aliyewatimua wasipande miti

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Mkoa wa Kilimanjaro na mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Grace Kiwelu ameeleza mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan namna viongozi wa baraza hilo la wanawake walivyodhalilishwa na kukataliwa kuotesha miche ya matunda katika Shule ya Sekondari Kiboriloni iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kiwelu amemweleza Rais Samia kuwa, Machi 3, mwaka huu walienda shuleni hapo kwa lengo la kuotesha miche ya matunda lakini walikataliwa na mmoja wa watumishi wa shule hiyo kwa kile alichoeleza kuwa mtumishi huyo aliwaeleza kuwa hawawezi kuotesha miche hiyo kwa kuwa wao siyo chama tawala.

Kiwelu ameyasema hayo leo mbele ya Rais Samia, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Mkoa wa Kilimanjaro ndani ya Ukumbi wa Kuringe uliopo Manispaa ya Moshi.

"Mheshimiwa Rais tunakupa heko kwa kulinda maadili katika nchi yetu, Mkoa wetu wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa ambayo ina joto kali sana, sisi wanawake wa Chadema tuliamua kufanya zoezi la kupanda miti ya matunda na vivuli ndani ya mkoa wetu," amesema.

"Tulifuata taratibu zote za maandalizi ambapo siku ya Ijumaa tulipanda miti katika Zahanati ya Merybenet katika Halmashauri ya Moshi DC, ingawa zoezi hili lilitanguliwa na upinzani mkubwa kutoka kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo na hatimaye lilifanikiwa baada ya uongozi wa serikali kuingilia kati na kutoa maelekezo," amesema.

"Mheshimiwa Rais, tulipofika Moshi tulikutana na upinzani mkubwa katika Shule ya Sekondari kiboriloni, tulifanyiwa unyanyasaji, tulinyimwa kuotesha miti Ile ambayo tulinunua kwa fedha zetu kutoka mifukoni mwetu," amesema.

"Mmoja kati ya watumishi wa shule Ile alitukatalia kwamba haturuhusiwi kuotesha miti Ile maana sisi siyo chama tawala, baada ya kupambana alisema hata yeye analinda ugali wake," amesema

"Kwa masikitiko makubwa tulilazimika kuondoka na miti yetu," amesema Kiwelu.
 
jingalo kabisa huyu..

Miti mbona maeneo mengi tu yasio ya serikali wanaweza kuotesha?

Mwambie Barabara ya Kwenda kwa Mkwe wake mbona ipo wazi haina miti?

Yaan Mkuu wa Nchi unamweleza utumbo wa aina hii? badala asimamie kuwatetea wananawake huko na mikopo ya H/ Anaongea kuzuiwa kuotesha mti[emoji23][emoji13]
 
Back
Top Bottom