Hao wanawake walishafukuzwa Chadema, hivyo kutumia jina lenye kiashiria cha chama walichofukuzwa sijawaelewa, hata kama wakisema wana kesi mahakamani, mpaka kwanza washinde hiyo kesi ndio watumie hilo jina, vinginevyo jina Chadema kwao kwa sasa sio sahihi.
Pamoja na hayo, naungana nao kwenye kuipigania Tanganyika yetu, tuikomboe kwa pamoja wote wenye mapenzi mema, kwani Tanganyika ndio mama yetu, vyama vya siasa vinafuata baadae.