beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,880
- 6,368
Klabu za soka za Real Madrid ya Uhispania na Bayern Munich ya Ujerumani zimefuzu kuenda hatua ya nusu fainali katika michuano ya [HASHTAG]#KlabuBingwaUlaya[/HASHTAG]
Pamoja na jana kufungwa goli 3-1, Madrid inafuzu kutokana na jumla ya magoli 4-3(aggregate) dhidi ya Juventus katika mechi mbili kwenye hatua ya robo fainali
Bayern yenyewe katika mchezo wa marudiano wa jana dhidi ya Sevilla ilitoka suluhu ya bila kufungana. Hivyo Bayern inafuzu kwa jumla ya goli 2-1(aggregate)
Timu nyingine zilizofuzu katika hatua ya nusu fainali ni Liverpool ya Uingereza na AS Roma ya Italia
Droo ya nusu fainali kujua Klabu gani zitakutana katika hatua hiyo itafanyika kesho, Ijumaa Aprili 13.